Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy
Mwalimu akielezea jambo katika kikao cha mwaka cha Wadau wa Sekta ya
Afya nchini mapema leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh.
Faustine Ndugulile akijibu hoja wakati wa kikao hicho cha Wadau wa Sekta
ya Afya, kilichofanyika mapema leo jiini Dar Es Salaam.
Kiongozi wa shirika la Maendeleo ya Afya Milma Kettunem(wa mwisho)
akiwasilisha mchango wake katika kikao cha Wadau wa Sekta ya Afya. Wa
kwanza ni Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu, na katikati ni Barozi wa
Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Waechter.
Wadau wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini taarifa kutoka kwa Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy
Mwalimu(hayupo kwenye picha) katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Afya
wenye lengo la kubainisha vipaumbele vya 2017/2018 katika Sekta ya Afya.
Na WAMJWW. DSM
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) leo ameongoza kikao cha mwaka cha Wadau wa
Sekta ya Afya nchini, huku lengo likiwa kujadili na kubainisha
vipaumbele vya mwaka 2018/2019 katika sekta ya Afya.
Akifungua
Mkutano huo Mh. Ummy Mwalimu(MB) alisema kuwa katika kuelekea Tanzania
ya Viwanda ni lazima taifa lielewe kwamba kuna umuhimu wa kuimarisha
Sekta ya Afya nchini katika ngazi ya utoaji huduma na miundombinu kwa
jamii ili kuwezesha uwepo wa jamii yenye afya njema itakayoweza
kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
“Ni Vigumu kutekeleza Sera ya Viwanda kama hatutaimarisha Sekta ya Afya nchini”, alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Katika
kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Wadau mbali mbali wa Maendeleo,
Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mashirika ya kidini na Sekta Binafsi
huku kikitawaliwa na masuala ya kuimarisha Afya ya mama na watoto
wachanga, rasilimali watu katika Afya, miundombinu ya Huduma za Afya,
rasilimali fedha katika Sekta ya Afya, Muendelezo wa Huduma, Utawala na
uwajibikaji na Afya ya vijana hasa wasichana.
Akiongea
kwa niaba ya Wadau wa Maendeleo, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania
Dkt. Detlef Waechter ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa nia ya dhati
katika kuimarisha na kukuza Sekta ya Afya nchini na kuahidi kuendeleza
ushirikiano ikiwemo kutoa rasilimali fedha na utawala ili kufanikisha
utoaji wa huduma bora za Afya katika jamii.
Kwa
upande wa Mashirika yasiyo ya kiserikali wameiomba Serikali kuharakisha
mpango wa Bima ya Afya kwa wote jambo litalosaidia kupunguza gharama za
matibabu kwa kiasi kikubwa kwa wananchi wa kipato cha chini.
0 on: " MH. UMMY MWALIMU AONGOZA KIKAO CHA MWAKA CHA WADAU WA SEKTA YA AFYA."