NA WAMJW-DAR ES
SALAAM
BAADHI
ya Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wanatakiwa kuhamia
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ili kuongeza rasilimali watu kwa ajili ya
kumudu hali ya ongezeko la wanaotaka huduma bora za afya hospitalini
hapo.
Hayo
yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu alipotembelea Hospitali hiyo ili kuangalis hali ya
utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hospitalini hapo.
"Kubwa
nliloligundua hapa ni kuna mlundikano wa idadi kubwa ya wanaohitaji huduma
hivyo wale madaktari tunaowatoa Muhimbili hasa madaktari bingwa baadhi
tutawahamishia hapa ili kusaidiana na madaktari wa Temeke katika kutoa huduma
bora kwa watu wengi zaidi" alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ipo mbioni kutafuta rasilimali fedha kwa
ajili ya kujenga jengo la ghorofa nne ambalo litachangia katika kuondoa tatizo
la mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo mapema mwaka huu.
Mbali
na hayo Waziri Ummy ametoa rai kwa wananchi wore kujiunga na mfuko wa Bima ya
Afya ili kupata huduma za matibabu kwa wakati sahihi na kwa bei nafuu hasa kwa
watoto wadogo wenye kadi inayoitwa Afya toto Kadi kwa bei ya shilingi 50, 400
tu.
Kwa
upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Amani
Malima amesema kuwa wapo mbioni kuagiza vifaa na vifaa tiba pamoja na kuomba
kuongezwa watumishi kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wengi zaidi kama
ilivyoelekezwa na Mhe. Waziri Ummy.
"Tunakabiliwa
na upungufu wa watumishi na ndo mana kuna mlundikano wengi wa wanaohitaji
huduma lakini tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuja na kuona changamoto zetu
na kutuhaidi mazuri zaidi katika jitihada za kutoa hufuma bora za afya kwa
wananchi" alisema Dkt. Malima.
0 on: "BAADHI YA MADAKTARI BINGWA KUTOKA MUHIMBILI WANATAKIWA KUHAMIA HOSPITALI YA TEMEKE KUONGEZA NGUVU. "