Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiwaonesha nembo ya MSD GOT inayotambulisha kuwa Dawa hiyo inatolewa
na Serikali kwa wananchi.
|
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akikagua moja kati ya Friji ya kuhifadhia chanjo.
|
WAMJW-KATAVI
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsioa,Wazee na Watoto Dkt.Faustine
Ndugulile amewataka wananchi kutumia nguvu
kazi yao katika ujenzi na uboreshaji wa Zahanati katika Wilaya zao
kuliko kupeleka pesa nyingi kwa wakandarasi.
Dkt.Ndugulile
ameyasema hao wilayani hapa wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya na
kutathimini shughuli za maendeleo
ikiwemo ya upanuzi wa miundombinu zikiwemo ya Zahanati
Alisema
kutumia nguvu kazi zao itasaidia kwa
kiasi kikubwa kupunguza gharama ambazo zingeweza kujitokeza kama wangetoa tenda
hiyo kwa wakandarasi.”Nyinyi ndio wasimamizi wakuu wa shughuli hizi na
mkiharibu tutakuja kuwalaumu nyinyi
Aidha,alisema
Serikali imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya huduma za afya nchini
kwa upande wa uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji, wodi ya wazazi,maabara
,wodi ya watoto pamoja na nyumba ya mtumishi kwenye vituo vya afya ambapo
ujenzi huo unaanza mara moja
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile ameendele kuwatoa hofu wananchi juu ya hali ya
upatikanaji wa dawa, huku akiwasisitiza wananchi wasiuziwe dawa zozote muhimu
kwani hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri maeneo yote na sasa ni wastani wa
asilimia 80.
“Katika
kituo cha Afya Kanoge, bajeti ya dawa imeongezeka kutoka Milioni 300 mpaka
Bilioni 2.5, kwahiyo dawa tunazo za kutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje
hapa aambiwe akanunue dawa sehemu nyingine, wamenithibitishia waganga wangu
asilimia 90 ya dawa muhimu zipo” aliendelea Dkt. Ndugulile
Wakati
huo huo Dkt. Ndugulile amesisitiza watumishi wa afya juu ya utunzaji wa
kumbukumbu za dawa katika stoo ya madawa ikiwemo kuweka za kujua idadi za dawa
zilizoingia na kutoka pamoja na utunzaji wa takwimu za mahudhurio ya wagonjwa wa
kila siku, jambo linalopunguza ufanisi katika kazi.
Hata
hivyo Dkt. Ndugulile amemtaka Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge
kuanzisha ofisi ya kushughulikia malalamiko ya watu pindi wanapokutana na
changamoto wakati wakipata huduma katika Kituo hicho cha Afya.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.
Yahaya Hussein wakati akiwasilisha taarifa ya Mkoa
alisema kuwa Mkoa wa Katavi unakabiriwa na uhaba mkubwa wa watumishi wa kada ya
Afya hali inayopelekea changamoto kubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Hadi
kufikia Septemba 2017 Mkoa wa Katavi una jumla ya watumishi 693 sawa na
asilimia 28 kati ya watumishi 2,437 wanaohitajika, kati ya hao 19 ni watumishi
ngazi ya Mkoa na 674 ngazi ya Serikali za mitaa, kwa ujumla Mkoa wa Katavi una
jumla ya upungufu wa watumishi 1,744” Alisema Dkt. Hussein.
Dkt. Yahaya Hussein
aliongeza kuwa Mkoa unaendelea kuzisimamia Halmashauri kuhakikisha zinatenga
bajeti kwa ajili ya kuwakatia kadi za Afya ya Jamii (CHF) wazee ili kuendelea
kupata Huduma za Afya kwa urahisi katika maeneo yao.
Mpaka
kufikia Mwezi Septemba 2017 jumla ya wazee 19,248 wametambuliwa, na kati ya hao
jumla ya wazee 1,807 sawa na asilimia 9.4 wameshapatiwa kadi za CHF katika
Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi.
0 on: "DKT NDUGULILE AWAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO."