Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipitia ramani ya jengo jipya la mama na
mtoto linaloendelea kujengwa katika hatua ya kuboresha huduma katika
kituo cha Afya cha Mazwi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiteta jambo na viongozi mbali mbali
katika moja ya jengo jipya linalojengwa ikiwa ni moja ya jitihada za kuboresha kituo cha Afya
cha Mazwi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiongoza msafala wa ukaguzi wa jingo
jipya katika kituo cha Mazwi Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akijiridhisha na uwepo wa Dawa katika stoo ya Dawa katika kituo cha Afya cha Mazwi.
Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
ndugulile akikagua Dawa katika stoo ya Dawa katika Kituo cha Afya Mazwi,
ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Rukwa wilaya ya
Sumbawanga, pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Boniface Kasululu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiwa ndani ya jingo jipya la wodi ya
kina mama wajawazito, katika ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa
katika kituo hicho.
Na WAMJWW. RUKWA-SUMBAWANGA
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha
wanapambana na kutokomeza udumavu kwa watoto unaosababishwa na ukosefu
wa Lishe bora.
Ameyasema hayo akiwa katika
muendelezo wa ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji huduma za Afya,
na uhamasishaji wa vikundi vidogo vidogo vya wanaweke vya ujasiriamali
katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
”Mkoa wa
Rukwa haupaswi kuwa na utapiamlo hata kidogo, asilimia 60 ya udumavu
ndani ya Rukwa ni kiasi kikubwa sana, katika mkoa ambao una chakula na
ardhi yenye rutuba nzuri ni jambo la kushangaza kuona tatizo hili”,
Alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea
kwa kusema kuwa, Siku 100 za mwanzo tangia mtoto anazaliwa ni muhimu na
nyeti sana katika kuhakikisha anapata maziwa ndani ya miezi sita, na
anapoanza kula ale vyakula vyenye lishe ya kutosha ili ubongo wake ukue
vizuri.
Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maelekezo kwa
sekretarieti ya Mkoa na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa pamoja
katika kutoa elimu ya kutosha kwenye kila mikusanyiko watakayofanya
kuhusiana na masuala ya Lishe bora ili kutokomeza janga hili
linalosumbua idadi kubwa ya watoto katika Mkoa huu.
Kwa
upande wake Mbunge wa Sumbawanga Mh. Aishi Hilaly amemshukuru Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile kwa kuwakumbuka katika mgao wa fedha za kuboresha
Vituo vya Afya cha Mazwi, pia hakusita kupaza sauti juu ya ombi la gari
la kubebea wagonjwa litakalosaidia kupunguza hadha kubwa wanayokumbana
nayo inayotokana na kukosekana kwa gari hilo.
Nae
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu Mkoa unaendelea kupambana na
magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoa elimu ya Afya
na Usafi wa mazingira kwa wananchi, ili kuhakikisha magonjwa haya
yanakuwa historia katika mkoa wa Rukwa.
Aidha, Dkt.
Kasululu alimuomba Dkt. Faustine kupunguza hadha ya upungufu wa
madaktari bingwa na mabingwa wa fani nyingine, Dkt. Kasululu alisema
kuwa hadi kufikia Desemba 2017 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa
inajumla ya madaktari bingwa 5 ambao ni sawa na asilimia 21 kati ya
madaktari 24 wanaohitajika.
0 on: " DKT. FAUSTINE AWAAGIZA VIONGOZI WA MKOA WA RUKWA KUTOKOMEZA UDUMAVU UNAOSABABISHWA NA LISHE DUNI"