NA WAMJW-DAR ES SALAAM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya imeandaa Muongozo wa matibabu nchini na orodha ya dawa
zote muhimu ili kuepukana na tatizo la usugu wa vimelea vya dawa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote
muhimu uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
"Ni
muhimu kila kituo cha afya kuwa na dawa za kutosha, vifaa na vifaa tiba lakini
ni lazima tuzingatie muongozo wa matibabu na orodha ya dawa kulingana na
ugonjwa fulani ili kuepuka tatizo hili" alisema Waziri Ummy
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa Muongozo huo umezingatia vigezo vyote vya kuweka dawa
ambazo zilikuwa hazipo katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya
ambazo zimepata uthibitisho kutoka Shirika la Afya la Dunia (WHO).
Aidha
Waziri Ummy amewapiga marufuku Bohari Kuu ya dawa ya Taifa MSD na Mfuko wa Bima
ya Afya wa Taifa (NHIF) kuagiza na kuandika dawa zilizo nje ya muongozo
uliozinduliwa leo ili kuondoa matumizi ya dawa yasiyo sahihi.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kila kituo cha afya ni lazima kiongozwe na
Tabibu na sio vinginevyo ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika
kituo cha afya husika.
Kwa
mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa itafika kipindi vituo vya afya ambavyo
havikizi vigezo vitafungiwa ili kuepuka usababishwaji wa vifo visivyo vya
lazima kwa watanzania.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi amesema kuwa
muongozo wa kutibu magonjwa mbambali
umezingatia
Orodha ya dawa ambazo zitakuwa zinatumika nchini kwetu kama dawa muhimu za
kutibu magonjwa hayo.
0 on: "SERIKALI YAJA NA MUONGOZO ILI KUPAMBANA NA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA. "