WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameridhishwa na utekelezaji wa
agizo la kuhamisha wagonjwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda
Hospitali ya Tiba na Taaluma Mloganzila.
Hayo ameyasema wakati alipotembelea
Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuangalia hali ya utoaji wa huduma pamoja na
utekelezaji wa agizo hilo alilolitoa wakati alipotembelea Hospitali ya Tiba na
taaluma Mloganzila mapema mwezi huu.
“Niliwaagiza MNH kuhamisha wagonjwa
waliopo kwenye jingo la Mwaisela kuaznia wodi namaba 3,4,5,6,7 na 8 isipokuwa
wagonjwa mahututi na wenye kesi maalumu ila nawapongeza wametekeleza agizo hilo
mara moja” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amewapongeza MNH
kwa kuwahamisha madaktari bingwa 15 15 na wauguzi zaidi ya 30 kwenda katika
Hospitali ya Mloganzila ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma sawa na inayotolewa
Muhimbili.
Mbali na hilo Waziri Ummy amesema kuwa
zoezi hilo limetoa nafasi ya kuwahamisha baadhi ya wagonjwa wa Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI) hususani watoto angalau vitanda 50 kupeleka kwenye
jingo la Mwaisela hospitali ya MNH.
“JKCI ni moja wapo ya Taasisi zinazotoa
matibabu ya upasuaji hasa ya moyo na ina upungufu wa majengo hivyo kutokana na uhamishwaji wa wagonjwa
jengo la Mwaisela tunawapa nafasi ya kupeleka vitanda 50 kwa ajili ya wagonjwa
wao waliofanyiwa upasuaji hususan watoto” aliongeza Waziri ummy.
Sambamba na hilo Waziri Ummy alipata
muda wa kwenda kumtembelea Mgonjwa alikuwa analalamika kwenye baadhi ya vyombo
vya habari ajulikanaye kwa jina la Maria (17) mkazi wa Masasi Mkoani Lindi kuwa
ana uvimbe mkubwa na akalizimika kuletwa katika Hospitali ya Taifa yMuhimbili.
“ Niliposikia habari ya Binti huyo
kwenye baadhi ya vyombo vya habari niliomba namba za wahusika na kuwaelekeza
waende Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hivi sasa anapata matibabu kwenye
taasisi ya Mifupa (MOI) na wanaendelea na juhudi za kumtibia ili kumrudsha
katika hali yake ya zamani” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alitoa rai kwa
Watanzania kuwa wanatakiwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa madaktari bingwa na
kuacha imani potofu kwa kwenda kwa waganga wa kishirikina kwa kuamini mgonjwa
atakuwa amerogwa ili kuepuka tatizo kuwa kubwa zaidi.
“Kwa mujibu wa madaktari wamesema kuwa
Maria alihudhuria hospitali hapo mara mbili na hakurudi tena kama ilitakiwa
afanye na badala yake akajikita zaidi kwenye tiba asili mpaka imesababisha
tatizo kuwa kubwa zaidi hivyo watanzania tunatakiwa kuwaamini zaidi madaktari
na kufuata maelekezo” alisema Waziri Ummy.
0 on: "WAZIRI UMMY ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA KUHAMISHA WAGONJWA MNH"