Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika kupata huduma
katika Taasisi ya Mifupa MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za
Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Cheti cha mmoja kati ya wagonjwa
waliofika kupata huduma za matibabu katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, katika
ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa
Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua utunzwaji na uhifadhi wa dawa, katika
Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa
huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza) akiteta jambo na viongozi wa Taasisi
ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za
Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo, wakatika ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo
Dkt. Respicious Boniface.
Na WAMJWW.DSM
Serikali kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya
Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu
(MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma
zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi,
Hayo yamesemwa leo na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiwa katika ziara yake ya kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa kwa
wananchi na taasisi hiyo.
“Serikali imewapa fedha, Bilioni 16 ya kununua
vifaa vyakutumika kwenye jingo lao jipya, watafunga mashine mpya za kisasa
pamoja na CT-Scan na MRI, Thieta pamoja na kufungua kitengo cha zarura jambo
litalopunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma”, alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameahidi kuendelea kushirikiana
na Taasisi hiyo katika kuhakikisha
wanaiwezesha zaidi ili kuweza kufanya upasuaji mkubwa ndani ya nchi jambo
litakalopunguza usumbufu kwa mwananchi mwenye kipato cha chini.
Aidha, Dkt. Ndugulile
aliupongeza uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya
katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za Afya kwa wananchi hali iliyosaidia
kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu ya
mifupa.
“Niupongeze uongozi wa
Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika
magonjwa yanayohusiana na mifupa jambo lililosaidia kupunguza wagonjwa wengi
sana kupata huduma nje ya nchi” alisema Dkt. Ndugulile.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kwa
kiasi kikubwa sana kwani Zaidi ya Asilimia 95 ya maradhi ya mifupa hutibiwa
katika Hospitali hiyo na asilimia zilizobaki huwapeleka nje ya nchi.
Dkt. Respicious Boniface
aliendelea kuishukuru Serikali kwa Msaada huo wa Fedha kwaajili ya kununua Vifaa vya MRI na CT-Scan na kuahidi vifaa
hivyo vitafika mapema ndani ya mwezi wa Nne, hivyo kazi ya kuwaudumia wananchi
itaanza mapema.
“Sababu kubwa ilikuwa ni
vifaa, sasa tayari Serikali kupitia Wizara ya Afya imekwisha toa fedha kwaajili
ya vifaa hivyo hivyo ndani ya mwezi wa nne vitakuwa vimekwishafika”, alisema
Dkt. Dkt. Respicious Boniface.
0 on: "SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 ILI KUIMARAISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII."