Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (mwenye tisheti ya mistari) akipokea maelekezo ya
ramani ya jingo jipya la Mama na Mtoto katika kituo cha Afya Nkomolo,
anaemfuatia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu na wa mwisho
ni Mhandisi Mwakyembe.
Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (MB) akikagua jokofu la Chanjo wakati alipotembelea
katika Kituo cha Afya cha Nkomolo kilichopo Nkasi Mkoani Rukwa wakati wa
Ziara yake ya kukagua Huduma za Afya Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (MB) akikagua Bin Kadi ambayo inaonesha idadi ya Dawa
zilizoingia na zilizobaki katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo
Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Majengo
Mhandisi Mwakyembe kutoka Ofisi ya Mkoa wa Rukwa.
Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiendelea na ziara yake katika kituo cha Afya
Nkomolo, anaemfuata ni Mhandisi Mwakyembe na Mbunge wa Nkasi kaskazini
Mh.Kessy Ally.
Na WAMJWW. RUKWA-NKASI
Serikali
yaanza kutumia mfumo wa nyota kupima huduma zitolewazo na Vituo vya
Afya, Hospitali na Zahanati nchini ili kupima utendaji kazi wa watumishi
wa Sekta ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo
Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya
kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kuamsha hali kwa
wananchi katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
“Tumeanza
utaratibu wa kutoa nyota katika vituo vya Afya, imeanzia nyota sifuri
mpaka nyota tano, sifuri maana yake kituo hicho hakifai kutoa huduma ya
Afya na nyota tano maana yake kinafanya vizuri sana” Alisema Dkt.
Ndugulile.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile
aliridhishwa na hali ya upatikanaji wa Dawa katika kituo hicho, hivyo
kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza kuwa hawapaswi kuuziwa dawa zote
muhimu kwani Serikali imeboresha hali ya upatikanaji wa Dawa katika
vituo vyote vya Afya nchini.
“Dawa
zote za msingi tunazo zakutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa
kutibiwa kisha aambiwe akanunue katika vituo binafsi, Hali ya
upatikanaji wa Dawa ni nzuri katika kituo hiki na ni asilimia 85 ”
aliendelea Dkt. Ndugulile.
Aidha,
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy aliupongeza uongozi
wa Mkoa kwa kusimia vizuri ujenzi wa kituo hicho, uliojumuisha Thieta,
Wodi ya mama na mtoto mochwari na maabara mpaka hatua ya kupaua kwa
jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 290 kwa kutumia nguvu kubwa ya
wananchi (fixed akaunti).
Akiwasilisha
taarifa ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu
amesema kuwa Mkoa wa Rukwa umeendelea kuboresha huduma za Afya ya mama
na mtoto katika maeneo ya vijijini kama juhudi za kupunguza tatizo la
vifo vya wanawake na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi.
Dkt.
Boniface aliendelea kusema kwamba, Zaidi ya vituo 214 kati ya 223
vilivyopo, vinatoa huduma muhimu za mzazi na mtoto jambo linalosaidia
kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto
wachanga licha ya upungufu mkubwa wa vituo hivyo.
Kwa
upande mwingine Dkt. Boniface Kasululu alisema kwamba Mkoa unaendelea
kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto katika vituo
vinavyotoa huduma za chanjo, Hadi kufikia Mwezi Novembe 2017 jumla ya
Watoto 48,494 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja walipewa chanjo, kati
ya watoto 50,245 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 96 jambo
lililoufanya mkoa kuvuka lengo la kitaifa la asilimia 90.
0 on: "SERIKALI YAANZA KUTUMIA MFUMO WA NYOTA KATIKA KUVIPIMA VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI NCHINI"