Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa kwanza
kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya
Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara na Chuo
Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo.
Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha Uuguzi
Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch. Benjamini
Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao kifupi
kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko
uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.
Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya Arch.
Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya sehemu ya
jengo la Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara
CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika leo mkoani
humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim Catherine na kulia
ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya Bw. Castro
Simba.
Baadhi ya Majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC Chuo Cha Maafisa Tabibu
Mtwara na CoTc yakiwa yamekamilika katika mradi wa ujenzi wa
Ujenzi,Upanuzi na ukarabati wa majengo ya chuo hiko na Chuo Cha maafisa
Tabibu mtwara yalipokaguliwa na wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya
Afya leo mkoani Humo.
Jengo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini
ambalo lipo kwenye ujenzi bado ambapo limegharimu kiasi cha shilingi
Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyoni
kuweza kutoa huduma za kibingwa.
NA WAMJW-MTWARA
SERIKALI
Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi Nadhra
kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na ujenzi katika
majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC) na Chuo cha Maafisa Tabibu
mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi zaidi.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba wakati wa ukaguzi wa
majengo hayo mkoani Mtwara.
"Majengo
haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha mwaka mmoja
kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo hayajakidhi
ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi mmoja"
alisema Bw. Simba.
Aidha
Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati na kujenga
majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo Hospitali ya
Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara (NTC), Chuo Cha
Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha Sumbawanga.
Kwa
upande wake Mratibu wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na Mratibu wa Mradi
huo kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joachim Catherine amesema kuwa mradi
huo uliofadhiliwa na Global Fund umehusisha ujenzi Wa mabweni matatu
yenye vyumba 120, Nyumba za watumishi nane katika chuo cha maafisa
tabibu. Katika na Chuo cha uuguzi Mtwara.
Aidha
Dkt. Catherine amesema kuwa Miradi yote imegharimu kiasi cha Shilingi
bilioni 3.3 za kitanzania na kulifanyika ukarabati na upanuzi Wa
madarasa, ofisi za wakufunzi, maktaba pamoja na maabara za vitendo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi Mtwara (NTC) Bw. Frolian Mbungu
amesema kuwa amefurahishwa na ukaguzi huo kwani utamfanya apokee majengo
kwa kujiamini na kuyatumia kwa ufasaha.
Aidha
wakaguzi hao kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na
Mipango Dkt. Edward Mbanga walitembelea jengo la wagonjwa Kutoka nje la
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo limegharimu kiasi cha
shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali
hiyo ni kuweza kutoa huduma za kibingwa.
0 on: "SERIKALI YAMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUMALIZIA MAJENGO YA CHUO."