JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TANGAZO LA UFADHILI-MARUDIO
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anawatangazia wanafunzi wote walioko vyuoni na
wale wote waliopata udahili wa masomo ya Uzamili katika fani za Afya kwa mwaka
wa masomo 2017/2018, kuwa muda wa
kuwasilisha maombi umeongezwa hadi tarehe 19/01/2018. Ufadhili huu ni kwa
ajili ya kulipiwa ada pamoja na posho ya utafiti pindi mwanafunzi anapokuwa
kwenye kipindi cha kufanya utafiti kama sehemu ya mafunzo yake. Kwa wanafunzi
waliokwisha wasilisha maombi yao, hawatakiwi kuomba upya.
Vigezo vilivyowekwa ni kama
ilivyoainishwa kwenye Tangazo la awali ambavyo ni :
1.
Raia wa Tanzania.
2.
Awe amedahiliwa chuoni kuanza masomo kwa mwaka wa kwanza
2017/2018
3.
Watumishi wa Afya wanaofanya kazi katika vituo vilivyo
wilayani/mikoani ambao baada ya mafunzo, aidha wanaweza kupangiwa vituo vya
kazi (hospitali za mikoa) au kurudi na kuendelea kufanya kazi katika vituo vyao
vya awali ambao utaalamu wao utakuwa unahitajika na awe ameruhusiwa na mwajiri
wake kwenda masomoni.
4.
Nyanja za Tiba ambazo ni za msingi katika utoaji wa
huduma za rufaa katika hospitali za Rufaa za mikoa kama Anaesthisiology,
Surgery, Neurosurgery, Obstetric and Gynaecology, Orthopaedic Surgery,
Emergency Medicine, Paediatric, Internal Medicine, Critical Care in Nursing na
Midwifery and Womens Health
5.
Nyanja za ubingwa (Specialities na Super-specialities)
katika hospitali za kitaifa (magonjwa ya moyo, figo, saratani n.k.) ili kujenga
uwezo wa ndani ya nchi katika jitihada za kupunguza wagonjwa wa rufaa
wanaotibiwa nje ya nchi.
6.
Awe na barua ya ruhusa ya masomo kutoka kwa mwajiri wake
(ambatanisha)
7.
Awe tayari kuingia mkataba wa kuitumikia Serikali kwa muda
usiopungua miaka 5 baada ya kuhitimu mafunzo.
8.
Mtumishi asiwe na ufadhili mwingine.
Aidha, kwa kuwa wanafunzi
wamesharipoti vyuoni, barua za maombi zipitishwe kwa Wakuu wa Vyuo kuthibitisha
kuwa mwanafunzi yuko chuoni, na kwa wale ambao bado wapitishe barua kwa Mwajiri
wao. Tangazo hili linahusu watumishi wa mwaka wa kwanza wa masomo 2017/2018 tu.
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 19/01/2018. Waombaji wote
watume maombi hayo kwa anuani ifuatayo ;
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto,
Chuo Kikuu Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya
Maendeleo ya Jamii
Jengo Namba 11,
S.L.P 743
40478, DODOMA
Imetolewa na;
Katibu
Mkuu - Afya
16/01/2018
Mnachelewa sana kutoa majina ya walipata ufadhili wa masomo,kwahiyo inakuwa kero huku mavioni,mjitahidi wizara mtoe kwa wakati,ili mtu ajijue amepata ama laa
JibuFuta