Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya,
akihutubia mapema leo wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu
watakaotoa Huduma ya Usingizi, tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Afya
na Sayansi Shirikishi MUHAS jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Dkt. Otilia Gowelle, akinyoosha mkono kama ishara ya kujitambulisha, wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu
watakaotoa Huduma ya Usingizi.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya
Shahada za mwanzo MUHAS ambae pia alimwakilisha Mkuu wa Chuo Prof. Mainem Moshi
akiwasilisha taarifa fupi ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS wakati
wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu watakaotoa Huduma ya Usingizi.
Mlezi wa Wanafunzi kutoka
Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Dtk. Edith Tarimo akiwasilisha
Taarifa mbele ya mgeni rasmi ambae ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Tukio la ufunguzi wa Mtaala
wa Kufundishia watu watakaotoa Huduma ya Usingizi, katika ukumbi wa Chuo cha
Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt.
Mpoki Ulisubisya, wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa Kufundishia watu watakaotoa
Huduma ya Usingizi, tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Afya na
Sayansi Shirikishi MUHAS jijini Dar es salaam.
Na WAMJWW-DSM.
Watumishi wa wa afya wa kutoa huduma za usingizi
wanahitajika zaidi nchini ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa wingi na ukaribu
zaidi mara zinapohitajika kwa wagonjwa wanaohitaji upasuaji kwa usalama katika
hospitali zetu .
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Mpoki
Ulisubisya wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa kufundishia watu watakaotoka na
Shahada ya Huduma ya Usingizi itakayotolewa na Chuo Cha Afya na Sayansi
Shirikishi MUHAS leo jijini Dar es salaam.
“Nawaagiza wenzetu wa MUHAS wahakikishe kasi ya kuandaa mtaala wa kufundishia
iongezwe na uletwe haraka ili kuweza
kupata wataalamu wa kutoa huduma za usingizi ili wakafanye kjazi kwenye
Hospitali za Rufaa za Mkoa” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kabla ya mtaala
huu kupitishwa hapo nyuma wagonjwa awalikuwa wanapata huduma za usingizi pindi
wanapohitaji kufanyiwa upasuaji kutoka kwa wataalamu waliopata mafunzo kwa
mwaka mmoja au waliojifunza kwenye sehemu zao za kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo wa Shahada za
Mwanzo MUHAS Prof. Mainem Moshi amesema kuwa tayari wameshapeleka mtaala wa
wahandishi wa vifaa tiba kwani wanahitajika takribani wahandisi elfu 8 nchini.
Aidha Prof. Mainem amesema kuwa kusimamishwa kwa
mtaala wa kufundishia shahada ya udhamiri kwa kozi za ukunga kumepeleka vifo
556 katika kina mama laki moja kwa wamama wanaojifungua hivyo Serikali ipo haja
ya kurudisha huu mtaala.
0 on: "WATOA HUDUMA ZA USINGIZI WANAHITAJIKA ZAIDI NCHINI."