Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akisikiliza
kwa umakini changamoto kutoka kwa mgonjwa, pindi alipotembelea Hospitali ya
Rufaa ya Mbeya, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake a kukagua Ubora wa huduma za
Afya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB)
akisalimiana na mgonjwa pindi alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, wa kwanza
ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Yahya Msuya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB)
akikagua Bin Kadi katika Stoo ya Dawa pindi alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake a kukagua Ubora wa huduma za Afya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wa
katikati) akiendelea na ziara yake ya kukagua Ubora wa huduma za Afya, pindi alipotembelea
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jinsia kutoka
Wizara Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Idara ya Maendeleo ya
Jamii Dkt. Julius Mbilinyi, Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo.
Na WAMJWW. MBEYA
Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yaendelea kujizatiti katika
kupambana na magonjwa yasiyo yakuambukiza ili kulilinda kundi kubwa la jamii ya
Watanzania.
Hayo yalibainishwa na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiwa katika ziara yake Mkoani Mbeya ya kukagua shughuli za utoaji wa
huduma za Afya na kutathimini shughuli za maendeleo ikiwemo upanuzi wa
miundombinu kama vile Vituo vya Afya na Shule.
Dkt. Ndugulile alisema kuwa
magonjwa yakuambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana kutokana na
mabadiliko ya mtindo ya Maisha, kutofanya mazoezi na hali ya ulaji usiofaa wa
wananchi wengi katika jamii.
“Serikali imezidi kuboresha
upatikanaji wa Huduma za magonjwa ya Saratani, mfano kupitia Hospitali ya Ocean
Road tulioipatia vifaa vya kisasa sana, sambamba na hilo tumeanza kufanya
upandikizaji wa Figo ndani ya Hospitali ya Benjamini Mkapa,” Alisema Dkt.
Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea
kusema kwamba, Serikali imewapeleka madaktari katika nchi za China na India ili
kuanza kufanya mafunzo ya upandikizaji wa Ini, hali itakayosaidia kupunguza
gharama kubwa kwa wananchi kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Aidha, Dkt. Ndugulile aliupongeza
uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Jijini Mbeya kwa kuendelea kuboresha utoaji wa
huduma za Afya kwa jamii katika
Hospitali hiyo ikiwemo
upatikanaji wa Dawa ambayo ni zaidi ya Asilimia 90, kuwatambua Wazee na
kuwapatia vitambulisha.
“Taarifa niliyoipata katika
Mkoa wa Mbeya upatikanaji wa Dawa zote muhimu na za Wazee ni zaidi ya Asilimia
90, na katika Mkoa huu wa Mbeya wamepiga hatua kubwa sana kwa kuweza kuwatambua
wazee wengi na kuwapa vitambulisho”, Alisema Dkt. Ndugulile
0 on: "SERIKALI YAENDELEA KUJIZATITI KATIKA KUPAMBANA NA MAGOJWA YASIYO YAKUAMBUKIZA."