|
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle kulia akisaini mkataba wa
ujenzi wa kitengo cha huduma za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali
ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam, kushoto
ni Naibu Balozi wa Israel nchini Kenya Bw. Michael Baror.
|
|
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle kulia akibadilishana mkataba
wa ujenzi wa kitengo cha huduma za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali
ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam na Naibu
Balozi wa Israel nchini Kenya Bw. Michael Baror. |
|
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle akiongea na Waandishi wa
habari hawapo pichani wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa kitengo cha huduma
za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya
Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali ya Tanzania na Israel
kupitia Wizara ya Afya.
|
|
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle kulia akimkabidhi zawadi Naibu Balozi wa Israel nchini Kenya Bw.
Michael Baror. Kushoto wakati wa wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa kitengo
cha huduma za Dharura na Mifupa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa uliofanyika kati ya Serikali
ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya.
|
Na WAMJW-DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesaini mkatba wa makubaliano ya ujenzi wa
jengo la huduma za dharura na mifupa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo
mkoani Dodoma kutoka Serikali ya Israel .
Akizungumza baada ya makubliano hayo eo jijini Dar es salaam Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle amesema kuwa mkataba huo umefanywa na
Serikali ya Tanzania na Israel kupitia Wizara ya Afya ili kuboresha huduma za
afya nchini.
"Licha ya kusaini mkatba wa ujenzi wa vitengo
hivyo vya huduma za dharura na Mifupa pia Serikali ya Israel imejitolea na
kufundisha wataalam wetu katika vitengo hivyo pindi ujenzi
utakavyokamilika" alisema Dkt. Gowelle.
Aidha Dkt. Gowelle amesema kuwa anaishukuru
Serikali ya Israel kwa kuingia mkataba wa ujenzi huo kwani utasaidia Hospitali
hiyo kutoa huduma za dharura kwa ubora na kiwango cha juu kulingana na mahitaj
ya wananchi.
Kwa upande wake Naibu Balozi wa Israel nchini
Kenya Bw. Michael Baror amesema kuwa
ujenzi huo utakamilika ndani ya mwaka
mmoja na miezi mitatu na kuanza kutoa huduma mara moja.
0 on: "SERIKALI YASAINI MKATABA WA UJENZI WA KITENGO CHA DHARURA NA MIFUPA."