Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 6 Februari 2021

DAWA ASILIA SASA KUWEKEWA MKAKATI YA KUPATIKANA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NA MADUKA YA DAWA ZA BINADAMU

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akisema jambo kwa wazalishaji wa dawa asilia (hawapo pichani) kwenye kikao kilichowakutanisha wazalishaji wa dawa asilia na watendaji kujadili namna bora ya kurahisisha upatikanaji wa dawa asilia kwa jamii.

Dkt. Paul Mhame Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya akisema jambo kwa wazalishaji wa dawa asilia (hawapo pichani) kwenye kikao kilichowakutanisha wazalishaji wa dawa asilia na watendaji kujadili namna bora ya kurahisisha upatikanaji wa dawa asilia kwa jamii.

Wazalishaji wa dawa asilia na wataalam wa afya wakiwa kwenye kikao cha kujadili namna bora ya kurahisisha upatikanaji wa dawa asilia ndani ya jamii


Na WAMJW - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeweka mkakati wa kusogeza karibu huduma za tiba asili kwa jamii ambazo sasa dawa hizo asilia zinawekewa mikakati ya kupatikana hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na maduka ya kuuza dawa za binadamu.

Hayo yamesewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi mara baada ya kufanya kikao na wazalishaji wa dawa hizo asilia nchini ambao dawa zao zimethibitishwa Usalama na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali  pamoja na Msajili wa Tiba Asili nchini na kukidhi vigezo vya kutumika kwa binadamu.

“Sisi watendaji tumeona ni muhimu kukutana ili tuweze kuweka mikakati ya kuhakikisha hizi dawa asili zinawafikia wananchini kwa urahisi zaidi”amesema Prof. Makubi.

Amesema kuwa tunasumbuliwa na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza hivyo ni lazima tutumie silaha (dawa asilia na za kisasa) zote ambazo ni salama zinaweza kusaidia wananchi kwa afya.

“Kuna hizi dawa asili zenye usalama, ambazo zimekuwa zikitumika kutibu magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambikiza hivyo ni lazima tuzisogeze karibu kwa wananchi kupitia mawakala, maduka ya madawa ya binadamu nata hospitalini kwa usalama ziweze kuwafikia wananchi” ameeleza Prof. Makubi.

Aidha Prof. Makubi amewataka wasomi na wataalam wa afya kwa ujumla kubadili mtazamo wao juu ya tiba asili kwa kuwa zimekuwa na mchango mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na kuwaasa wataalam kutokuwa kikwazo kwa wananchi kutumia tiba asili.

“Kama dawa sisi tumeshaihakiki na tukaikubali kwamba hii dawa ni salama, basi pasiwepo na kinyongo au ugumu wowote wa sisi watumishi wa afya kuruhusu mwananchi kutibiwa kwa dawa hiyo ”Amesisitiza Prof. Makubi.

Katika hatua nyingine Prof. Makubi hakusita kuwaasa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kinga za magonjwa magonjwa yote ikiwemo kufanya mazoezi, kubadili mtindo wa maisha na kula chakula bora. Wananchi siyo lazima wasubiri matamko ya Serikali katika kujikinga na magonjwa; njia nyingi za kujikinga na magonjwa zimeshatolewa na wanazijua; kwa hiyo ni suala la wao kujenga mazoea ya kujikinga kila siku ya Mungu.

Prof Makubi alielezea pia umuhimu wa kufanya tafiti zaidi katika tiba asilia ili ziweze kuhakikia kwa miongozo ya nchi na kimataifa na baadae kuweza hata kuhudumia wananchi wa nchi za jirani. Aidha alisisitiza kuwa Wagunduzi watalindwa na Serikali na kuhakikisha umiliki wa ugunduzi wa dawa hizo haupotei wakati na baada ya utafiti. 

Naye Dkt. Paul Mhame, Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa Serikali kupitia Taasisi zake imeweza kuchambua na kuidhinisha dawa za kunywa aina 5 na dawa aina 4 za  mafuta tete  kwa ajili ya kujifukiza ambazo zimekidhidi vigezo kuweza kutumika kwa binadamu. Amezitaja dawa hizo za kunywa kuwa ni NIMRICAF, COVIDOL, BINGWA, PLANET ++ pamoja na COVOTANZA huku zile za mafuta tete zikiwa ni BUPIJI pamoja na UZIMA. 

“Aidha Serikali inaendelea kufanya kazi kwa karibu na wazalishaji wengine ambao wakikidhi vigezo dawa zao zitaongezwa kwenye orodha hii” Amesema Dkt. Mhame na kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwenda kununua dawa hizo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa ambukizi na yasiyoambukiza.

Akizungumuza kwa niaba ya wazalishaji wa dawa asili Bw. George Buchafwe ambaye ametengeneza dawa ya kujifukiza kwa mafuta tete ya Bupiji ameishukuru Serikali kwa kuona mchango wao na kuwa sehemu ya kuchangia na kuboresha afya za wananchi. 

“Tunaishukuru Serikali kwa kutambua kuwawapo watafiti ambao wanaweza wakaisaidia jamii yetu na ikawezakutoka katika hatua kwenda hatua nyingine kwa kutumia tiba zetu za asili” Amesema Bw. Buchafwe.

Amesema kuwa wao wazalishaji wa dawa za asili wapo tayari kushirikiana na Serikali kuzalisha bidhaa bora ye usalama kwa afya ya binadamu.

Kwa upande wake Dr Otieno kutoka Taasisi ya Tiba Asilia Muhimbili amesisitiza umuhimu wa wananchi kuacha kuchanganya dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja wakati wa kutumia. Amesema ni vema pia wananchi wafuate maelekezo sahihi ya matumizi ya hizi dawa na kuzingatia usalama wake.

Alhamisi, 4 Februari 2021

TAASISI NA VYUO VYA AFYA ZATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUBORESHA TIBA ASILI NCHINI

 

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bw. Edward Mbaga akisema jambo kwa viongozi wa taasisi na vyuo vya afya nchini kwenye kikao cha kuboresha tiba asili nchini

Viongozi wa taasisi na vyuo vya afya nchini wakisiliza wasilisho la mada kwenye kikao kazi cha kuboresha tiba asili nchini.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ema jambo kwa viongozi wa taasisi na vyuo vya afya nchini kwenye kikao cha kuboresha tiba asili nchini
Na Englibert Kayombo, WAMJW - Dodoma

Taasisi za Sekta ya Afya na Vyuo vya afya nchini vimetakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuboresha tiba asili ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kupambana na magonja ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Wito huo umetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Bw. Edward Mbaga alipokuwa akifungua kikao kazi cha viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya na Vyuo vya taaluma ya afya nchini kilicholenga kuboresha ushirikiano na kuangalia namna ya kuongeza rasilimali katika kuboresha tiba asili nchini.

“Tumekutana hapa ili kuwa pamoja tujadili jinsi ya kushirikiana katika kupata frdha za kugharamia uzalishaji na kufanya tafiti za kutambua usalama, ubora na ufanisi wa dawa za tiba asili nchini” amese Bw. Mbaga wakati akifungua kikao kazi hicho.

Amesema kuwa Jamii imekuwa ikitumia huduma za tiba asili kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali na baadhi ya wananchi wanatumia huduma zote mbili kwa maana ya tiba ya kisasa na tiba asili katika kutibu magonjwa.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha utoaji wa huduma hizi kwa kuhakikisha Jamii yetu inaatumia dawa salama, yenye ufanisi na ubora katika kulinda afya ya jamii kwa ujumla, hili linawezekana kwa kufanya tafiti za kina kwa dawa zetu”amesisitiza Bw. Mbaga.

Amesema kuwa Serikali imekwisha tambua tiba asili kuwa na umuhimu toka mwaka 1969 ambapo ilielekeza Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya tafiti za miti dawa ili kuweza kuleta Ushahidi wa kisayansi na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu usalama, ubora naufanishi wa dawa za asili ambazo kwa Tanzania kuna zaidi ya miti dawa 12,000 ambayo inatibu magonjwa mbalimbali.

Aidha Bw. Mbaga amezitaka taasisi zote zinazohusika katika mausala ya tiba asili kushirikiana kwa pamoja ili kuja na majibu yanayoleta tija kwa taifa na kusaidia upatikanaji wa dawa za asili yenye manufaa kwa watanzania na ulimwengu kwa ujumla.

“Taasisi zinafanya tafiti lakini tatizo lililopo hapa ni kwamba kila taasisi inafanya kazi peke yake na kusababisha tafiti nyingi kujirudia rudia, hii inasababisha matumizi ya rasilimali ndogo zilizopo kutotumika kwa mapana kuweza kufanya tafiti nyingi tofauti na kuleta tija kwa jamii” ameeleza Bw. Mbaga.

Naye Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amesema kuwa ni lazima viongozi wote wa taasisi na vyo vya afya nchini kuwa na mtazamo chanya juu ya tiba asili kuwa zinaweza kusaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali

“Ni muhimu kuunganisha mawazo yetu sisi viongozi na wasomi mbalimbli ili tuweze kuonyesha kwamba sisi wenyewe wasomi tunatambua mchango wa tiba asili katika nchi yetu kwa ajili ya kukinga na kutibu magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza” amesema Prof. Makubi

Amesisitiza kusema kuwa dawa zote za asili ni lazima zifanyiwe utafiti kabla ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya matumizi na ili kufanikisha hilo ni lazima tuwe na rasilimali za kutoka kuwezesha kufanya tafiti za kina juu ya dawa hizo za asili.

“Mheshimiwa Rais amekwisha toa maelekezo ya bajeti ya afya kuongezwa kwenye upande wa tiba asilia, pamoja na kuunganisha nguvu za Serikali, lakini pia taasisi bado zina uwezo wa kuchangia kuhakikisha tafiti kwa ajili ya tiba asili zinafanyika”Amefafanua Prof. Makubi

Mwisho