Taasisi za Sekta ya Afya na Vyuo vya
afya nchini vimetakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuboresha tiba asili ambayo
imekuwa na mchango mkubwa katika kupambana na magonja ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
Wito huo umetolewa leo na Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Bw. Edward Mbaga alipokuwa akifungua kikao kazi cha
viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya na Vyuo vya taaluma ya afya
nchini kilicholenga kuboresha ushirikiano na kuangalia namna ya kuongeza
rasilimali katika kuboresha tiba asili nchini.
“Tumekutana hapa ili kuwa pamoja
tujadili jinsi ya kushirikiana katika kupata frdha za kugharamia uzalishaji na
kufanya tafiti za kutambua usalama, ubora na ufanisi wa dawa za tiba asili nchini”
amese Bw. Mbaga wakati akifungua kikao kazi hicho.
Amesema kuwa Jamii imekuwa ikitumia
huduma za tiba asili kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali na baadhi ya
wananchi wanatumia huduma zote mbili kwa maana ya tiba ya kisasa na tiba asili
katika kutibu magonjwa.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha
utoaji wa huduma hizi kwa kuhakikisha Jamii yetu inaatumia dawa salama, yenye ufanisi
na ubora katika kulinda afya ya jamii kwa ujumla, hili linawezekana kwa kufanya
tafiti za kina kwa dawa zetu”amesisitiza Bw. Mbaga.
Amesema kuwa Serikali imekwisha
tambua tiba asili kuwa na umuhimu toka mwaka 1969 ambapo ilielekeza Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya tafiti za miti dawa ili kuweza kuleta Ushahidi wa
kisayansi na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu usalama, ubora naufanishi wa
dawa za asili ambazo kwa Tanzania kuna zaidi ya miti dawa 12,000 ambayo inatibu
magonjwa mbalimbali.
Aidha Bw. Mbaga amezitaka taasisi zote
zinazohusika katika mausala ya tiba asili kushirikiana kwa pamoja ili kuja na
majibu yanayoleta tija kwa taifa na kusaidia upatikanaji wa dawa za asili yenye
manufaa kwa watanzania na ulimwengu kwa ujumla.
“Taasisi zinafanya tafiti lakini
tatizo lililopo hapa ni kwamba kila taasisi inafanya kazi peke yake na
kusababisha tafiti nyingi kujirudia rudia, hii inasababisha matumizi ya
rasilimali ndogo zilizopo kutotumika kwa mapana kuweza kufanya tafiti nyingi tofauti
na kuleta tija kwa jamii” ameeleza Bw. Mbaga.
Naye Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Abel Makubi amesema kuwa ni lazima viongozi wote wa taasisi na vyo vya afya
nchini kuwa na mtazamo chanya juu ya tiba asili kuwa zinaweza kusaidia katika kutibu
magonjwa mbalimbali
“Ni muhimu kuunganisha mawazo yetu
sisi viongozi na wasomi mbalimbli ili tuweze kuonyesha kwamba sisi wenyewe
wasomi tunatambua mchango wa tiba asili katika nchi yetu kwa ajili ya kukinga
na kutibu magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza” amesema Prof. Makubi
Amesisitiza kusema kuwa dawa zote za
asili ni lazima zifanyiwe utafiti kabla ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya
matumizi na ili kufanikisha hilo ni lazima tuwe na rasilimali za kutoka
kuwezesha kufanya tafiti za kina juu ya dawa hizo za asili.
“Mheshimiwa Rais amekwisha toa
maelekezo ya bajeti ya afya kuongezwa kwenye upande wa tiba asilia, pamoja na
kuunganisha nguvu za Serikali, lakini pia taasisi bado zina uwezo wa kuchangia
kuhakikisha tafiti kwa ajili ya tiba asili zinafanyika”Amefafanua Prof. Makubi
Mwisho
"This article highlights the importance of [topic, e.g., career counseling for students]. As a college, your dedication to student development and Summons With Notice Divorce New York education is commendable. Resources like this are invaluable for preparing students for the future. Great job supporting academic and personal growth.
JibuFuta