Msimamizi wa kitengo cha Afya katika
Shirika la Maendeleo ya Afrika (NEPAD) yenye makao makuu yake nchini Afrika ya
Kusini Bi.Margareth Ndomondo akiongea wakati wa uzinduzi huo.Shirika hilo
katika afya linasaidia kupunguza magonjwa yanayoikabili nchi za Afrika.(Picha zote na Wizara ya Afya)
Na.WAMJW-DAR ES SALAAM
TANZANIA ni miongoni mwa nchi inayotumia
dawa zilizo salama na ubora wa hali ya juu barani Afrika kutokana na udhibiti
na umakini unaofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mamlaka wa
Udhibiti na ubora wa dawa barani afrika
unaofanyika jijini Dar es Salaam.
”Sisi kama
Tanzania tunafanya vizuri sana katika udhibiti wa madawa yanayoingia,nataka
niwathibitishie kwamba Tanzania dawa
zetu tunazozitumia ni salama na zipo salama kwa uhakika mkubwa” alisema Dkt.
Ndugulile
Aidha ,Dkt.
Ndugulile alisema kuwa ongezeko la matumizi ya dawa ambayo hayana kiwango na
kutumika katika mfumo wa tiba umeleta changamoto katika kuongeza gharama za
matibabu nchini na barani Afrika
Kwa mujibu
wa Dkt. Ndugulile amesema changamoto hizo zinasababisha wagonjwa wengi kukaa
hospitalini,kuongeza gharama, kuathiri matokeo ya mgonjwa na hatimaye vifo
pamoja na kuleta usugu wa dawa kwa kutumia dawa zisizo na kiwango
Hata hivyo Dkt.
Ndugulile alisema mkutano huo utajenga utaratibu na mfumo wa pamoja wa kuona ni jinsi gani wanaweza
kudhibiti matumizi ya madawa yasiyo na kiwango barani afrika.
“Nataka niwathibitishie Watanzania kwamba tuna
dawa za kutosha na dawa zote zinazoingia
zina ubora unaotakiwa,Taasisi yetu ya TFDA inatambulika Kimataifa, ina viwango
vya Kimataifa na tumeboresha maabara zetu kuwa za kisasa na kutumika katika
bara la afrika katika udhibiti wa madawa”.
Alisema Dkt. Ndugulile.
Naye kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi.Agnes Kijo alisema mamalaka
hiyo imejidhatiti katika masuala ya udhibiti wa dawa hivyo kupelekea mkutano
huo kufanyika Tanzania
“Maabara
yetu hivi sasa imewekewa vifaa vya kisasa ambapo mwaka huu wa fedha ilitengewa
shilingi bilioni tano nukta moja kwa
ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya maabara ya Dar es Salaam na kanda ya ziwa ambapo itasaidia kufanyiwa
uchunguzi wa dawa katika ukanda uliopo na hivyo kutoa majibu kwa wakati na
mamlaka kufanya maamuzi sahihi” alisema Bi. Kijo.
Mkutano huo
ambao una lengo la kubadilishana uzoefu wa
masuala mbalimbali yanayo uhusiana na udhibiti na ubora wa dawa ambapo
kumekuwa na changamoto za matatizo ya madawa yasiyo na kiwango umekutanisha
nchi zipatazo 17 na utafanyika kwa siku
tano.
|
0 on: "TANZANIA INATUMIA DAWA ZILIZO SALAMA KWA UHAKIKA MKUBWA"