Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 27 Februari 2018

TANZANIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.


Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.


Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi.

Wadau wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB)  wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.


Na WAMJW - Dar es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 ili kuondoa tatizo hilo nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.

“Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani, kuimarisha afya ya wanawake Tanzania pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi mwaka huu”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Hata hivyo alisema hivi sasa hakuna takwimu za kitaifa ila kwa  takwimu toka vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na  taasisi ya Saratani ya Ocean Road,"kwa mwaka 2016/2017 saratani ya shingo ya kizazi ni  Asilimia 32.8 huku ikifuatiwa na saratani ya matiti kwa asilimia 12.9"

Alisema kati ya wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti na vifo vitokanavyo na saratani kwa akina mama ni asilimia 50 ambapo chanzo ni saratani ya shingo ya kizazi na matiti.

Aidha,Waziri Ummy alisema Serikali imepanga kuanza kuwapatia chanjo hiyo wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri wa chini na jumla ya wasichana 616,734 watapatiwa chanjo hiyo.
Aidha,Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka mabinti wao kwenye chanjo hivyo kwani ni salama na itatolewa kwenye vituo vyote vya afya vya Serikali vipatavyo 7,000,mashuleni pamoja na huduma za afya za vikoba bila malipo.
Naye Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Dafrossa Lyimo  amewatoa hofu wananchi na kusisitiza juu ya umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya Duniani (WHO)na itatolewa na wahudumu wa afya waliopata mafunzo.

0 on: " TANZANIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE"