Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akimtazama mtoto njiti, aliyepakatwa na mamaye, wakati
alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika
Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akiongea na mama Mjamzito wakati alipofanya ziara ya kukagua
hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa
Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akieleza Waandishi wa Habari (hawapo kwenye picha) umuhimu wa
kifaa kinacho rekodi mahudhurio na muda wa watumishi kufika ofisini
(Biometric) wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za
Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyetoka kujifungua, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwaMganga Mfawidhi, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Hospitali
teule ya Mkoa wa Pwani Tumbi, baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua
hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
HOSPITALI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUWA NA ICU YA WATOTO WACHANGA
NA WAMJW - PWANI
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ameziagiza Hospitali za rufaa zote nchini kuwa na ICU kwaajili ya watoto
wachanga ili kupunguza vifo vifo vyao.
Waziri
Ummy amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa
huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri
Ummy ameagiza hayo kupitia kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kuwa
ahakikishe watoto wachanga lazima wawe na ICU yao ili kuhakikisha vifo
vya Watoto wachanga vinapungua nchini.
"Watoto
wachanga wagonjwa, wawe na ICU yao, lengo letu kama Serikali ni
kupunguza Vifo vya Watoto wachanga, kwasababu tukipunguza vifo vya
Watoto wachanga, tutakuwa tumepunguza vifo vya Watoto wanye umri wa
chini ya miaka mitano" alisema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto
wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, hivyo
Serikali inaendelea kuchukua jitihada za makusudi ili kupunguza vifo
hivi, ikiwemo kusisitiza kila Hospitali nchini kuwa na ICU.
"Karibu
40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100,
Watoto 40% ni Wachanga, kwahiyo Daktari ni lazima tulifanyie kazi agizo
hilo" alisema Waziri Ummy.
Licha
ya changamoto alizokutana nazo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali
inatarajia kujenga jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura katika
Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ili kuokoa maisha ya wagonjwa,
hasa waliopata ajali.
"Nafurahi
kusema, Serikali imeahapata fedha kwahiyo tutakuwa na jengo mahususi
kwaajili ya huduma za Dharura na wagonjwa wa ajali, na hii tunataka iwe
katika Hospitali za Rufaa za Mikoa zote ili mgonjwa aweze kuokolewa
maisha muda mfupi anapofika Hospitali" alisema Waziri Ummy.
Pia,
Waziri Ummy ameridhishwa kwa kiasi kikubwa juu ya hali ya upatikanaji
wa dawa nchini, huku akiwatoa hofu Mwananchi kuwa Serikali kupitia
Bohari ya Dawa (MSD) ina dawa zakutosha.
Aliendelea
kusema kuwa Serikali imeainisha fani nane nane za kipaumbele ili kuwa
na madaktari Bingwa wawili katika kila fani ikiwemo, Daktari Bingwa wa
Watoto, Daktari Bingwa wa magonjwa yakina mama na uzazi, Daktari Bingwa
wa upasuaji wajumla, Bingwa wa upasuaji wa mifupa, Daktari Bingwa wa
magonjwa ya ndani (Physician) n.k
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika Mkoa wa Pwani Serikali imejenga
na kuboresha vituo vya Afya zaidi ya 16, Hospitali za Wilaya 3, na
kuboresha Hospitali ya Mikoa ili kuwa na huduma za wagonjwa mahututi na
wagonjwa wa Dharura.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amewahasa Mwananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya
Afyà ili kujihakikishia matibabu wakati wa ugonjwa, jambo litalosaidia
kuokoa gharama kubwa za matibabu pindi Mwananchi anapopata ugonjwa.
"Nitoe
Wito kwa Wananchi kujenga utaratibu wakujiunga na Bima ya Afya,
kwasababu ndio njia ya uhakika yakujihakikishia matibabu kabla
hawajaugua" alisema Waziri Ummy.
Mwisho.
0 on: " HOSPITALI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUWA NA ICU YA WATOTO WACHANGA"