Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akijiandaa kupanda mti, wakati wa zoezi la upandaji miti katika
Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya lililo katika mji wa Serikali
katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akimwagilia maji mti wake aliopanda, wakati wa zoezi la
upandaji miti lililo fanywa na Watumishi wa Wizara ya Afya katika mji wa
Serikali ulio kata ya Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Zainab Chaula akimwagilia maji mti alioupanda katika Mazingira ya
Wizara ya Afya, yaliyo katika Mji wa Serikali uliopo katika kata ya
Mtumba jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akiweka mbolea
katika mti wake, katika Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililo katika mji wa Serikali uliopo
katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (Wakatikati) akiteta jambo na
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku (Wakulia) na Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi (Wakwanza kushoto)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akifanya ukaguzi wa jengo la Wizara ya Afya lililo katika hatua
ya mwisho, leo wakati wa zoezi la upandaji miti katika Mazingira ya
jengo la Wizara ya Afya lililo katika mji wa Serikali katika kata ya
Mtumba jijini Dodoma.
Muonekano wa jengo la Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto lililo katika mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba
jijini Dodoma, jengo hilo liko katika hatua ya mwisho ya ujenzi,
Na WAMJW - DOM
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu leo
amewaongoza Watumishi wa Wizara ya Afya katika zoezi la upandaji miti
katika mji mpya wa Serikali ulio katika kata ya Mtumba, tarafa ya
Kikombo Jijini Dodoma.
Katika
zoezi hilo Waziri Ummy ameagiza Watumishi wote waliohusika katika
upandaji wa miti hiyo kuhakikisha wanaitunza vizuri isitawi, na ameagiza
kila mtu kuchukua jukumu hilo.
"Hii
miti ambayo tumeipanda sio tu miti ya kivuli na mapambo tu, bali
imejumuisha miti ya matunda. Miti hii ambayo tunaipanda ili ikue na
kustawi, lazima kila mtu, ambae amepanda mti wake kuhakikisha kwamba
haufi" Alisema Waziri Ummy.
Mbali
na hayo, Waziri Ummy amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab
Chaula kutenga maeneo kwa ajili ya Watumishi kufanya mazoezi ikiwa ni
mpango wa Serikali ya awamu ya Tano kupambana na Magonjwa yasiyo
yakuambukiza.
"Mazingira
ya hapa ni mazuri kweli kutembea, ukizunguka huu mji hukosi Kilomita 5,
nitamwandikia Waziri Jenister atusaidie kuwa na mabafu kwa ajili ya
watu wanaofanya mazoezi kubadilisha nguo jioni, ni lazima sehemu za kazi
ziwe rafiki kwa watu kufanya mazoezi" alisema Waziri Ummy.
Kwa
upande mwingine, Waziri Ummy amempongeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula na
kikundi chake kwa kuja na wazo la upandaji wa miti katika mji huo, na
kuwa mfano wa kuigwa na Wizara nyingine.
Katika
zoezi hilo lililojumuisha viongozi mbalimbali wa wizara, jumla ya miti
470 imepandwa katika awamu ya kwanza, lengo ikiwa ni kupanda miti 525.
Miti 320 iliyopandwa ni ya matunda, na mingine ni kwa ajili ya mapambo
na kivuli.
0 on: "WAZIRI UMMY AWAONGOZA WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA KATIKA ZOEZI LA UPANDAJI MITI"