Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akipokea vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa
katika vituo vya Afya hapa nchini, kutoka kwa Mkuu wa Masuala ya Afya
UNICEF Kyaw Aung, (Wakwanza kushoto) tukio limefanyika katika Ofisi
ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Pembeni kwa Waziri Ummy ni
Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari wakati akipokea
majokofu ya kutunzia chanjo na vishikwambi (tablets) kwaajili ya
kukusanyia taarifa katika vituo vya Afya hapa nchini, tukio limefanyika
katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Wakatikati ni
Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi, na Wakwanza kushoto
ni Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.
Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung akieleza jambo mbele ya
Waandishi wa Habari katika mapokezi ya majokofu ya kutunzia chanjo na
vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa katika vituo vya
Afya hapa nchini, yaliyofanywa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (wakatikati) tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akipokea majokofu ya kutunzia chanjo, kutoka kwa Mkuu wa
Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung (Watatu kushoto) tukio limefanyika
katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Kulia kwa
Waziri Ummy ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi,
Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi na Meneja wa Mpango wa chanjo
Taifa Dafrosa Lyimo.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati akipokea majokofu ya
kutunzia chanjo na vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa
katika vituo vya Afya hapa nchini, tukio limefanyika katika Ofisi ndogo
za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
SERIKALI YAWAHASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO
Na WAMJW – DSM
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
leo amewahasa Wazazi na Walezi nchini kuakikisha wanawapeleka watoto
kupata huduma za chanjo ili kujikinga dhidi ya maradhi yanayozuilika kwa
chanjo.
Waziri Ummy
amesema haya leo wakati akipokea majokofu ya kutunzia chanjo na
vishikwambi (Tablets) kwa ajili ya kukusanya taarifa za chanjo katika
vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.
Waziri
Ummy alisema kuwa imethibitika kuwa yapo magonjwa zaidi ya 20 nambayo
yanadhibitika kwa njia ya chanjo hivyo ni muhimu kwa wazazi na walezi
ambao hawajawapeleka watoto kupata chanjo kuitumia fursa hii ili watoto
wao wapate chanjo
“Sasa
hivi imeshathibitika kuna magonjwa zaidi ya 20 ambayo yanadhibitika
kupitia njia ya chanjo , ni lazima wahakikishe Wazazi ambao
hawajawapeleka watoto wao kupata chanjo , ni lazima wapate tena dozi
zote.” Alisema Waziri Ummy.
Waziri
ummy, alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na shirika la gavi,
imefanikiwa kununua jumla ya majokofu 1,385 yenye thamani ya shilingi
bilioni 13,991,270,300, huku ikichangia kwa 20% na gavi 80%, kwa ajili
ya kuimarisha mnyororo baridi wa utunzaji wa chanjo katika vituo vya
kutolea huduma za afya hapa nchini.
Aliendelea
kusema kuwa Majokofu 1,190 yanatumia nishati ya jua na kila jokofu lina
thamani ya shilingi milioni 10,879,000 na majokofu 195 yanatumia umeme,
na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 5,361,000.
Vilevile
Waziri ummy alisema, Serikali na shirika la Gavi imenunua jumla ya
vishikwambi (tablets) 1,249 vyenye gharama ya shilingi bilioni
1,598,720,000 kwa ajili ya kukusanya na kuhifadhi taarifa za chanjo kwa
njia ya mtandao, na kila kishikwambi kina thamani ya shilingi milioni
1,280,000.
Aidha, Waziri
Ummy alisema kuwa mapema mwezi Mei tutapokea jumla ya vishikwambi 2100
venye thamani ya shilingi bilioni 2,688,000,000 na mwishoni mwa mwaka
huu, tutapokea awamu nyingine ya majokofu yenye thamani ya shilingi
bilioni 11,533,357,820 na kufikia asilimia zaidi 80 ya mahitaji ya
majokofu na vishikwambi katika vituo vyote hapa nchini.
Mbali
na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa Halmashauri zote za Tanzania Bara
pamoja na Wilaya za Zanzibar zitapokea majokofu haya kwa awamu kuu
mbili, ambapo Awamu ya kwanza itahusisha mikoa 15 ambayo ni Dodoma,
Geita, Kagera, Kigoma, Lindi, Tanga, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza,
Shinyanga, Songwe, Unguja, Pwani na Singida huku awamu ya pili
itahusisha mikoa iliyobaki.
Hata
hivyo, katika kuhakikisha ufanisi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa
majokofu ya kuhifadhia chanjo, Wizara ya Afya kwa kushikiana na wadau wa
shirika la JSI na Nexleaf kwa ufadhili wa Gavi, inatarajia kufunga
vifaa vya kupima na kufuatilia halijoto katika vituo takribani 5,000
kati ya vituo zaidi ya 7,000 kote nchini.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa, Vifaa hivi vinamuwezesha Afisa Chanjo
kujua utendaji kazi wa jokofu ikiwa ni pamoja na kujua halijoto ya
jokofu katika vituo vya huduma za afya bila ya kulazimika kufika katika
kituo husika, Vifaa hivi vinatuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pindi
halijoto inapopanda au kushuka.
Mwisho.
0 on: " SERIKALI YAWAHASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO"