Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi kadi ya Bima ya Afya Bw. Said Akili kutoka AMCOS ya Nyundo B iliyopo Halmashauri ya Nanyamba kijiji cha Nyundo, wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipitia majarada ya wateja wanalioomba kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya, wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi, na muitikio wa Wakulima kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua idadi ya watu walioingizwa kwenye mfumo ili kupata kadi za Bima ya Afya, wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi, na muitikio wa Wakulima kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara na Lindi.
Na WAMJW - MTWARA
Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameuagiza
uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutatua changamoto ya uchelewaji
wa vitambulisho vya bima ya afya kwa wananchi.
Ameyasema hayo
mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utendaji kazi wa mfuko
huo Mkoa wa Mtwara, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji
huduma za Afya Mkoani hapo.
DKt. Ndugulile
amesema kuwa NHIF ni lazima ihakikishe inawahudumia vizuri wananchi wanaokuja
kujiunga katika mfuko huo, ikiwemo kuhakikisha ndani ya wiki mbili baada ya
kujaza fomu, wateja wapate kadi zao.
"Tuendelee
kuwahudumia vizuri, na kuhakikisha kwamba, ndani ya wiki mbili baada ya kujaza
fomu na kukamilisha taratibu, waweze kupata kadi zao" alisema DKt.
Ndugulile
Pia, Dkt.
Ndugulile amesema Serikali imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na mwitikio mzuri wa wananchi
kujiunga na Bima ya Ushirika jambo litalowasaidia kupata huduma za afya katika
vituo takribani 6,000 nchi nzima.
Aidha, Dkt.
Ndugulile ameagiza NHIF kuweka utaratibu wa kuwafuata na kuwapatia kadi za bima
wateja waliojiandikisha ili kuweka hamasa kwa wananchi wengine kujiunga na bima
ya afya na kuwapunguzia usumbufu.
Mbali ya hayo DKt.
Ndugulile ametoa onyo kwa watoa huduma za afya wanaofanya udanganyifu, na
kuwataka watoe huduma kwa kufata sheria, na kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya
Afya,
DKt. Ndugulile
aliendelea kusema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za maboresho ya sheria
ambazo zitatoa adhabu kali kwa yeyote atakayehusika na udanganyifu wowote
utaopelekea hasara kwa Serikali.
Kwa upande mwingine
DKt. Ndugulile amewaagiza watoa huduma za afya kuhakikisha wanawasilisha madai
yao kwa NHIF kwa wakati, huku akisisitiza kuwa NHIF nayo inapaswa kulipa madeni
kwa wakati.
"Haipendezi
wananchi wanahudumiwa katika vituo vyetu vya kutolea huduma za Afya, na madai
yanakaa zaidi ya miezi miwili au mitatu, kwahiyo niombe watoa huduma
waharakishe madai yao, ili waweze kulipwa kwa wakati" alisema DKt.
Ndugulile.
Nae Mkulima wa
Korosho kutoka Halmashauri ya Nanyamba kijiji cha Nyundo, amewataka wakulima
kupitia vyama vya Ushirika wajiunge na Bima ya Afya ili kuepuka gharama kubwa
za matibabu na ugonjwa hauchagui muda wa kuja.
"Nimehamasika
kujiunga na bima ya afya baada ya kuelewa kwamba ukulima una muda wa kupata
pesa na una muda wa kukosa, alafu homa haichagui muda," alisema Bw. Said
Akili.
Aidha Bw. Said
Akili ameiomba Serikali kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya hasa kwa
Wateja wanaotumia kadi za Bima ya Afya, jambo litalo wahamasisha wakulima wengi
zaidi kujiunga na mfuko huo.
0 on: "NHIF YATAKIWA KUTOCHELEWESHA KADI ZA WANACHAMA"