Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akikata utepe, ishara ya ufunguzi rasmi wa uzinduzi
wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika
katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi
wa NIMRI Prof. Yunus Mgaya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwajulia hali wagonjwa waliokwisha fanyiwa upasuaji
wa Mabusha baada ya kufanya uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu
wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni
Kigamboni.
Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (jayupo kwenye
picha) wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa
Mabusha, uliofanyika katika Hospitali ya Vijibweni Kigamboni.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wananchi waliojitokeza
kumsikiliza (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa kambi ya
upasuaji kwa watu wenye ugonjwa wa Mabusha, uliofanyika katika Hospitali
ya Vijibweni Kigamboni.
Mratibu wa Mpango wa taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Upendo Mwingira akitabasamu, baada yakupata pongezi kutoka kwa Naibu
Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile, kwa kazi nzuri anayoifanya ya
kutokomeza Matende na Mabusha.
Madaktari kutoka Hospitali ya Vijibweni Kigamboni wakifanya upasua wa
kutoa busha leo, katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye
ugonjwa wa Mabusha, uliofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine
Ndugulile (Hayupo kwenye Picha)
HALMASHAURI ZATAKIWA KUWEKA MIKAKATI THABITI ILI KUTOKOMEZA UGONJWA WA MABUSHA.
Na WAMJW – DSM
NAIBU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ameziagiza Halmashsuri zote nchini kuhakikisha
zinaweka mikakati thabiti ili kutokomeza Magonjwa ya Matende na Mabusha
nchini.
Ameyasema hayo
leo wakati wa Uzinduzi wa kambi ya upasuaji kwa watu wenye tatizo la
ugonjwa wa Mabusha na kuangalia hali ya utoaji Huduma za Afya katika
Hospitali ya Vijibweni Manispaa ya Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam.
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa Halmashsuri zote nchini wakati zinaandaa
Vipaumbele ni lazima watenge bajeti kwaajili ya mipango endelevu ili
kuhakikisha kwamba zinaweza kupambana na Magonjwa haya yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele bila kuwategemea Wafadhili.
“Niwaombe
sana, Wakati mnaandaa Mipango hii, tusiweke masuala mengi ya Semina,
tuelekeze nguvu katika intervention, tuweke vitu ambavyo vitaleta
mabadiliko, tutenge fedha kwaajili ya mipango endelevu, kwaajili
yakuhakikisha kwamba tunaanza kujisimamia katika Magonjwa haya,
haipendezi kama nchi kwenda kulia kwa Wafadhili kwa mambo ambayo
tunaweza kuyafanya” Alisema Dkt. Ndugulile.
Mbali
na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa, kati ya Wilaya 120 ambazo
zilikuwa na uambukizo wa magonjwa haya, Wilaya 96 zimeweza kupunguza
maambukizi kwa asilimia 80, hivyo kufikia kiwango cha kusimamisha
ugawaji wa Kingatiba kwa jamii katika Wilaya hizo.
Dkt
ndugulile aliendelea kuwahasa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kushiriki
kikamilifu pindi yanapotokea mazoezi kama haya ili tuweze kutokomeza
ugonjwa wa Matende na Mabusha, kwani bado Mkoa wa Dar es Salaam,
maambukizi yapo juu kwa kiwango cha asilimia 10.
Aidha,
Dkt ndugulile amesema kuwa Watu wapatao 206,708 sawa na asilimia 87.47
katika Manispaa ya Kigamboni walipatiwa Kingatiba, na kwa Manispaa ya
Ubungo Watu wapatao 997,632 sawa na asilimia 87.36 walipatiwa Kingatiba,
huku manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam, jumla ya watu wapatao
5,127, 596 sawa na asilimia 87.63 walipatiwa Kingatiba hiyo.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali kupitia uhisani wa
CNTD, inatarajia kuwafanyia upasuaji watu 400 wakazi wa Manispaa za
Kigamboni na Ubungo huku akiwaomba Wananchi wa Manispaa hizo kujitokeza
ili kutumia vizuri fursa hii adimu.
Nae
Mratibu Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa Serikali kupitia Mpango huu
kwa kushirikiana na Wadau inatoa huduma hii ya upasuaji kwa wagonjwa
hawa bila malipo, hivyo kuwahasa watu wenye ugonjwa huu kujitokeza ili
kupata huduma hii.
Nae
Shuhuda aliyepata huduma hii ya upasuaji Bw. Ahmed Abrahaman amewahasa
Watu wengine walio na ugonjwa huu kujitokeza kupata huduma hii ya
upasuaji ili kuondokana na aibu hii kwa jamii, huku akisisitiza kuwa
upasuaji huu unafanyiwa kwa njia za kisasa na wa muda mfupi sana.
0 on: " "