Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Bella Bird ambaye aliongozana na mtaalam kutoka ofisi ya Benki ya Dunia hapa nchini Ndg. Inaam Al Huq na Mariam Ally.
Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara Dkt. Leonard Subi, masuala mbalimbali yameongelewa ikiwemo Mradi unaoendelea kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia uitwao "Uimarishaji wa Afya ya Msingi na hususani katika kuzuia vifo vya mama na mtoto".
Vile vile, wameongelea miradi mipya miwili yenye lengo la kuboresha na kuimarisha Huduma za Lishe wenye lengo la kupunguza udumavu pamoja na mradi wa kupunguza vifo vya akina Mama Wajawazito nchini.
Miradi hiyo itatekelezwa kwa namna mbalimbali ikiwemo kuhakikisha Watoto wote wanaotakiwa kusoma wapelekwe shuleni na kuwepo na programu za kuwawezesha wanapata vyakula wakiwa shuleni.
Pia, katika mradi wa kuokoa vifo vya Mama na Mtoto, mradi utalenga kwenye uimarishaji wa miundombinu wa Vituo vya Afya pamoja na upatikananaji wa huduma bora kwenye vituo vyote.
0 on: "WAZIRI UMMY AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA"