Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia daftari la matibabu kutoka kwa moja kati
ya wazazi waliopeleka watoto wao kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji
huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akimsalimia moja Kati ya Wazee waliofika kupata
huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala,
wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika
Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akifanya ukaguzi katika chumba cha kuhifadhia Dawa
wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala,
wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika
Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongea na moja kati ya wazazi waliopeleka watoto
wao kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala,
wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika
Hospitali hiyo.
SEKTA YA AFYA ISIWE KIKWAZO KWA WANANCHI KUPATA MATANGAZO YAO MAPEMA.
Na WAMJW - DSM
NAIBU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ameagiza Sekta ya Afya kutokuwa kikwazo kwa wananchi
kupata Matangazo ya kuzaliwa kwa watoto kwa ajili ya kupata cheti cha
kuzaliwa kwa muda mfupi.
Ameyasema
hayo leo, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za
Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala jijini Dar ea
salaam.
Dkt. Ndugulile
amesema kuwa Hospitali hiyo ni lazima ichukue juhudi za makusudi,
ikiwemo kuongeza wafanya kazi ili kuhakikisha kwamba Watoto wote
wanaweza kupata matangazo yao ndani ya Wiki moja, jambo litaloepusha
usumbufu kwa Mwananchi ambao unaweza kuepukika.
"
Sisi kama sekta ya Afya, tusiwe kikwazo, vya Mwananchi kupata haya
matangazo, na hili nimeliona nimeshatoa maelekezo juu ya hili, na ndani
ya wiki moja nategemea kwamba tatizo hili litakuwa limetatuliwa" Alisema
Dkt. Ndugulile
Dkt.
Ndugulile akiongeza kuwa Matangazo haya ni ya muhinu sana katika
mchakato wa kupata vyeti vya kuzaliwa, hivyo Mganga Mfawidhi ni lazima
aweke mikakati thabiti ikiwemo kuongeza watu ili kuhakikisha kuanzia
sasa matangazo yawe yanatoka ndani ya masaa 24.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupambana na
changamoto ya msongamano wa watu katika Hospitali hiyo, Serikali
imeboresha zaidi ya vituo vya Afya 350, huku zikijengwa Hospitali za
Wilaya 67, na Hospitali za mikoa 2, ili wananchi waweze kupata huduma
katika ngazi ya chini kabla yakufikia katika Hospitali za Rufaa.
"Kama
Serikali tunachofanya ni kuboresha vituo vya Afya karibia 350,
tunajenga Hospitali za Wilaya 67, na Hospitali za Rufaa za Mikoa 2,
hivyo tunatarajia hizi Hospitali zinkianza kufanya kazi na huduma za
upasuaji zikianza kupatikana kule, huu msongamano utaamia kule" alisema
Dkt. Ndugulile
Mbali na
hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza watu wote wenye VVU kujitokeza kupata
matibabu, huku lengo la Serikali ni kufikia 909090, yaani 90 watu wote
walio na Virusi vya Ukimwi waweze kufikiwa na kupimwa, 90 ya pili ni
kuhakikisha waliopimwa waweze kuanzishiwa dawa papo kwa papo, na 90 ya
tatu ya walioanzishiwa dawa waweze kufubaza virusi vyao vya Ukimwi, yote
ni kuhakikisha ifikapo 2030 pasiwe na maambukizi mapya ya virusi vya
Ukimwi.
Nae Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dkt. Mkungu
Daniel mesema kuwa Hospitali hiyo inapokea Mwananchi zaidi ya 2000, huku
akisisitiza kuwa Hospitali hiyo ipo katika hatua yakujenga jengo ambalo
litabeba jumla ya vitanda 150 kwaajili ya mama na mtoto ili kupambana
na changamoto hiyo ya msongamano
0 on: "SEKTA YA AFYA ISIWE KIKWAZO KWA WANANCHI KUPATA MATANGAZO YAO MAPEMA"