Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu (Wapili kushoto) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.
Assumpter Mshama (wakwanza kushoto), pamoja na Wataaalamu wa masuala ya
ujenzi, wakiendelea na ukaguzi wa kiwanda cha Dawa cha Kairuki
Pharmaceutical Ltd katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu (Wapili kushoto) akimueleza jambo Mwekezaji wa Vista
Pharmaceutical Ltd, wakati wa ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa
Viwanda vya Dawa katika unaoendelea katika Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akisistiza jambo, kulia kwake ni Mwekezaji wa kiwanda cha dawa Vast Pharma Ltd.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu baada ya ziara ya kutembelea
Viwanda vya Dawa vya Vista Pharma Ltd na Kairuki pharmaceutical Ltd
vinavyojengwa katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
(Picha 1) Muonekano wa Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Ltd na na
Ofisi yake (Picha 2) unaoendelea kujengwa katika Wilaya ya Kibaha Mkoa
wa Pwani.
UJENZI WA VIWANDA VYA DAWA KUOKOA MABILION YA SHILINGI NCHINI
Na WAMJW - PWANI
WAZIRI
Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
leo amefanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa kiwanda vya Dawa
cha Vista Pharma Ltd na Kairuki Pharmaceutical Ltd vinavyoendelea
kujengwa kwa kasi katika Mkoa wa Pwani.
Katika
ziara hiyo Waziri Ummy alilenga kujionea na kutatua Changamoto
zinazowakumba Wawekezaji nchini hususani katika Viwanda vya Dawa ili
kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachoendelea kupotea kutokana na
kuagiza Dawa nje ya nchi.
Waziri
Ummy amesema kuwa katika kila Shilingi 100 ambayo Serkkali inatumia
kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, Shilingi 94 inapotea nje ya nchi,
ambapo kumalizika kwa Viwanda hivi kutasaidia pesa hiyo kubaki ndani ya
nchi na kutumika katika shughuli nyingine za Maendeleo kwa Wananchi.
"Katika
kila Shilingi 100 ambayo Serikali inatumia kununua Dawa, Vifaa na Vifaa
Tiba, Shilingi 94 tunaipeleka nje ya nchi kununua Dawa, Vifaa na Vifaa
Tiba, na ndiomaana nimefanya ziara hii pamoja na viongozi wa Mkoa na
kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Kituo cha uwekezaji ili kuokoa
fedha hiyo inayopotea nje ya nchi" alisema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy aliendele kusema kuwa kumalizika kwa Viwanda hivi kutasaidia kwa
kiasi kikubwa upatikanaji wa Dawa za kutosha na kwa bei rahisi, jambo
litalosaidia kuimarika kwa huduma za Afya nchini.
"
Dawa kupatikana kwa wingi na kwa bei rahisi na kwa haraka zaidi,
kwasababu kuagiza Dawa nje ya nchi MSD anatumia mpaka miezi 6 mpaka
ifike Tanzania" alisema Waziri Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy amewaagiza Tanesco ndani ya Mkoa kuhakikisha wanaleta
huduma ya umeme ndani ya wiki moja ili hatua za mwanzo za ufungaji wa
mashine katika Viwanda hivyo uanze Mara moja.
Pia,
Waziri Ummy amewaagiza Mamlaka ya Maji Mkoani Mkoa wa Pwani kuhakikisha
wanaleta huduma ya maji ndani ya Machi 15 katika eneo hilo la Viwanda
ili kuharakisha shughuli za ujenzi.
Mbali
na hayo, Waziri Ummy amewashukuru wawekezaji hao wa Ndani kwa maamuzi
mazuri aliyochukua ya kuwekeza katika Viwanda vya Dawa ili kuisaidia
Jamii ya Watanzania ambao Dawa bado imekuwa ni changamoto licha ya
Jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali katika kukabikiana na changamoto
hiyo.
#TunaboreshaAfya
A completely new and crisp feel with fiery letters and lovable flames that pop up lifeless of night|at 메리트카지노 midnight} background. This elegant theme in dark colours is soothing to the eyes, and the color selection units the temper for a fiendishly fun time. You can log in and utilize the bank button to make your preliminary deposit after your account has been reconciled.
JibuFuta