Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 14 Februari 2020

MAAFISA AFYA WATAKIWA KUIMARISHA UKAGUZI KWENYE MIPAKA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenye jengo la mpaka wa nchi ya Uganda ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kuangalia utayari wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

 Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akiongea na watumishi wa idara mbalimbali wa mpaka wa mtukula nje ya jengo la kituo cha pamoja nchini Tanzania.





Dkt. Chaula akiangalia ofisi ya maofisa afya wa mpaka wa mtukula nchini Tanzania na kujionea jinsi wanavyotoa huduma ikiwemo ya kudhibiti magonjwa ya milipuko na utoaji wa chanjo ya homa ya manjano(Yellow Fever).


MAAFISA AFYA WATAKIWA KUIMARISHA UKAGUZI KWENYE MIPAKA

Na. Catherine Sungura-Kagera

Maofisa afya wanaofanya kazi kwenye mipaka nchini  wametakiwa kuongeza umakini  wa  kufanya ukaguzi katika mipaka.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainab Chaula wakati alipotembelea mpaka wa Mutukula nchina Tanzania na Uganda ikiwa ni moja ya ziara yake ya kuangalia utayari wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo inafanywa na wizara ya afya kwa kushirikiana na TAMISEMI.

"Umakini mkubwa unatakiwa katika kufanya ukaguzi kwa wasafiri wanaopita kwenye.mpaka huu ingawa kuna mwiingiliano mkubwa baina ya nchi hizi mbili ili kuweza kuzuia magonjwa ya mlipuka kama Ebola usiingie nchini.

"Kujilinda ni jambo moja na kuzuia ni jambo lingine,nimetembelea mpaka huu, nimejionea na maofisa wetu wa Tanzania wa afya, forodha, uhamiaji wamenieleza changamoto iliyopo hapa ni mwingiliano mkubwa, watu wanatoka upande mmoja kwenda mwingine kwa wingi, wanashirikiana kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi,hivyo lazima muangalie tunatoka vipi kwenye hili.

Hata hivyo Dkt. Chaula aliwapongeza watumishi wote wa idara zote kwa ushirikiano na kwa kazi kubwa waliyoifanya  katika kudhibiti magonjwa ya milipuko hayajaingia  nchini.

"Lakini pamoja na hayo, bado inahitajika muwe imara zaidi, ndiyo maana tumeleta vifaa tiba  vya kisasa vya ukaguzi wa joto la afya ya mwili, nawasihi msimamie hili kwa umakini zaidi," alisema.

Aidha, Dk. Chaula alisisitiza maofisa afya hao kuongeza elimu.ya afya kwa umma kwa wananchi wote wanaopita mpakani hapo ili kuwajengea uelewa  jinsi ya kujikinga na dalili  za magonjwa hayo

"Wataalamu wa afya wa Mkoa na viongozi wote pamoja hakikisheni elimu ya afya kwa umma  inafika hadi kule vijijini, watu wetu waelewe jinsi ya kujikinga," alisema Dk. Chaula.

MWISHO

0 on: " MAAFISA AFYA WATAKIWA KUIMARISHA UKAGUZI KWENYE MIPAKA"