Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 12 Septemba 2019

FUATILIENI MTOTO ALIYEKATWA MKONO MWANANYAMALA: DKT. NDUGULILE


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokua akiongea wakati wa uzinduzi wa bodi ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa hoteli ya Veta jijini Dodoma.Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Vivian Wonanji akiongea na washiriki waliohudhuria uzinduzi wa bodi hiyo


Msajili wa baraza la maabara binafsi za afya Dominic Fwiling'afu akiongea wakati wa uzinduzi.huo.
Kaimu Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Said Abood akitoa neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa bodi ya maabara binafsi za afya ambapo aliahidi kufanya ukaguzi wa kuzibaini maabara ambazo hazijasajiliwa nchini.


Aliyekuwa mjumbe wa bodi iliyoisha muda wake Dkt. Charles Massambu akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile
Kaimu Msajili wa bodi ya Maabara binafsi Dickson Majige akipokea cheti cha shukrani wakati wa uzinduzi huo.


Baadhi ya wasajili wa mabaraza ya kitaaluma yaliyo chini ya wizara ya afya wakimsikiliza Naibu Waziri(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo.

Picha ya pamoja mgeni rasmi na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.

Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akiwa kwenye picha ya pamoja na bodi mpya ya nane ya baraza la maabara binafsi za afya.
Na. Catherine Sungura –Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee wa Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Msajili wa  Baraza la Madaktari la Tanganyika kushirikiana na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania kufuatilia mtoto aliyekatwa mkono baada ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mwananyamala.

Dkt. Ndugulile ametoa maagizo hayo wakati akizindua bodi ya nane ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa Veta jijini hapa.
“Nilitegemea baraza la madaktari muwe mmeanza uchunguzi, kwahiyo nakupa maagizo kesi hiyo muanze kufuatilia na kama itathibitika ni uzembe waliohusika wachukuliwe hatua, ndani ya wiki mbili mtuletee majibu ili mimi na Mhe. Waziri tujue tunachukua hatua gani.

Dkt. Ndugulile amesema kwenye mabaraza bado kuna changamoto ya baadhi ya mashauri kuchukuliwa hatua hivyo kama mabaraza ya kitaakluma ni vyema kuangalia ufanisi wa majukumu yao na kuchukulia hatua pale taaluma inapokosewa na waliokosea wachukuliwe hatua.

Dkt. Ndugulile ameitaka bodi hiyo kusimamia usajili wa maabara zote nchini kwani hivi sasa imetokea uanzishwaji wa maabara kiholela zinazotoa huduma kwa wananchi bila ya kusajiliwa hivyo kufanya ukaguzi ili kubaini maabara hizo na kuzichukulia hatua.

“Naomba sheria ifuate mkondo wake ili kubaini wale wote walioanzisha huduma za maabara bila kufuata sheria na taratibu za usajili, tushirikiane kuhakikisha kuwa hakuna taasisi au mtu atakayefungua au kutoa huduma za maabara bila kusajiliwa”. Amesisitiza Dkt. Ndugulile.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema baraza hilo ni chombo muhimu na ndio moyo wa sekta ya afya kwani maabara inatoa muelekeo wa mgonjwa kwa kuthibitisha tatizo, hivyo inahitajika maboresho katika utoaji huduma za maabara. 

“Sasa hivi huduma hizi zimekua ni biashara kwani asiliamia 70 ya homa wala sio Malaria ni virusi watu wanakunywa dawa sana pasipo kuzingatia misingi kwani maabara hizi zinatumika kama sehemu ya matibabu na hata upasuaji, mtu anaenda maabara anakaa dakika kumi na tano anaambiwa ana UTI wakati mwingine anaambiwa ana malaria plasi plasi hii maana yake ni nini hili linahitaji ufuatiliaji”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Hata hivyo aliitaka bodi hiyo mpya  kusimamia ubora wa huduma za maabara  ili kuinufaisha jamii na kuhakikisha huduma za afya katika jamii zinaboreshwa kukidhi viwango vitavyotarajiwa na hivyo kuboresha afya na maisha ya watanzania.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la maabara binafsi Prof. Said Abood  aliahidi kutekeleza maagizo yote waliyopewa na Naibu waziri ikiwemo ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini maabara bubu na  ambazo hazijasajiliwa pamoja na kuhakikisha maabara zinatoa huduma zinazostahili ili kuweza kumsaidia daktari kumpatia mwananchi huduma stahili.

-Mwisho-

0 on: "FUATILIENI MTOTO ALIYEKATWA MKONO MWANANYAMALA: DKT. NDUGULILE"