Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wakati
akitoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini
Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Amref Afrika Dkt. Floriance Temu
akiongea na waandishi wa habari wakati maazimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula
Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia
idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon akiongea na waandishi wa habari mbele
ya Waandishi wa habari na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Na WAMJW-DSM.
WANAWAKE
wajawazito wanatakiwa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo
ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano
wa kupata ugonjwa wa Fistula.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika
kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.
“Asilimia
60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili
mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula
hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40 tu
ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha,
Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia
Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua
idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.
Vilevile
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya
vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo
nayo ni sababu inayopelekea kwa wanamke kupata fistula.
Hata
hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma za Fistula zinapatikana Bure nchini
hasa kwenye hospitali za CCBRT,Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana
dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya
na kupata ushauri.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linayoshughulikia mambo
ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula
nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali za Wilaya na Mkoa.
Naye
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA
Bi. Jacqueline Mahon amesema kuwa
Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili
kupamabana na ugonjwa huo.
“Mbali
na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya
,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula
na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” alisema
Bi. Mahon.
Mbali
na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji hospitali ya CCBRT inashirikkiana na Serikali
katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa
wagonjwa 1500 kila mwaka .
Ugonjwa
wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba
kauli mbiu isemayo “BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA
NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”
0 on: "WANAWAKE WAJAWAZITO WANATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI MARA KWA MARA KUZUIA FISTULA."