Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Esther Jason mwongozo wa Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi vitendea kazi Mkemia Mkuu wa Serikali Fidelice Mafumiko wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar
es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Esther akiongea akitoa neno mbele ya viongozi wa Serikali na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulileakisisitiza jambo mbele ya Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mku na viongozi wengine wa Srikali wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar
es salaam.
Na WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeitaka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua hatua
ya kupima maji yanayotiririka mitaani kutoka viwandani kubaini kama yana
kemikali ambazo zinaathiri wananchi au hazina madhara yoyote.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afy, Maendeleo ys Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya
Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar
es salaam.
"Bodi hii
ninayoizindua leo inatakiwa kuhakikisha majibu ya watu wanaokuja kuleta
vipimo vyao yatoke mapema na haraka iwezekanavyo ili kupunguza
msongamano wa wateja wenu" alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Mamlaka hiyo inatakiwa kushirikiana na
kufanya mazungumzo na Taasisi ya Chakula na Dawa TFDA na TBS ili
kutoingiliana katika majukumu kwani kuna kuna kipengele cha majukumu yao
kinafanana katika kusimamia ubora wa chakula.
Aidha
Dkt. Ndugulile ameitaka Mamlaka hiyo kuisimamia kikamilifu sheria ya
uchafuzi wa Mazingira ili kuepusha wananchi na magonjwa ya kuambukiza na
yasioambukiza.
Kwa
upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo
Dkt. Fidelis Mafumiko amesema kuwa wanaiomba Serikali kutatua changamoto
ya upungufu wa mitambo ya kufanyia kazi katika mamlaka hiyo.
Aidha
Dkt. Mafumiko amesema kuwa Bodi hiyo iliyozinduliwa leo ipo tayari
kufanya kazi kwa manufaa ya Watanzania japo mamlka hiyo ina upungufu wa
Watumishi kutoka watumishi 400 mpaka kufikia watumishi 220.
Bodi
ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imezinduliwa leo ikiwa
na Wajumbe saba ambao ni Mwenyrkiti wa bodi hiyo Prof. Esther Hellen,
Katibu Dkt. Fidelis Mafumiko, Dkt. Eliud Eliakimu, Dkt. Samwel
Gwamaka, Dcp. Hussein Laiser, Bi. Irene Leisure na Bw. Pius Mponzi.
0 on: "MAJI YANAYOTIRIRIKA MITAANI KUTOKA VIWANDANI YAPIMWE KEMIKALI. "