Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine
Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma
za Afya katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma, Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt.Pamela Sawa.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine
Ndugulile akimkabidhi cheti cha shukrani kwa aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya
Ushauri wa Hospitali za watu binafsi
Dkt.Mohamed Ally Mohamed katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine
Ndugulile akizindua kanuni za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi
katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara
hiyo Dk Otilia Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt.Pamela Sawa.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine
Ndugulile akizindua Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma
za Afya katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu
Wizara hiyo Dk Otilia Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi
Dkt.Pamela Sawa.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine
Ndugulile akimkabidhi cheti cha shukrani kwa aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya
Ushauri wa Hospitali za watu binafsi
Dkt.Mohamed Ally Mohamed katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.
Na WAMJW-DODOMA
Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mfumo mpya wa TEHAMA wa kusajili
vituo vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali ikiwa na lengo
la kuboresha mfumo wa kujisajili ambapo waombaji wapya watafanya maombi
yao kupitia mfumo huo popote walipo na kufuatilia maombi hayo popote
walipo kupitia mfumo huo.
Hii
ni tofauti na hapo awali ambapo muombaji alilazimika kusafiri kufika
wilayani, mkoani na hata kufika Taifa yaani kwa msajili wa hospitali
nchini.
Uzinduzi huo
umefanywa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo, Jijini Dodoma ambapo pia alizindua
kanuni za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi, mwongozo wa
viwango vya msingi kwa vituo vya kutolea huduma za afya nchini pamoja
uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali za watu binafsi.
*“Nina
uhakika maombi ya usajili wa vituo vya afya sasa yataenda kwa haraka.
Waombaji watajaza fomu na kulipia hukohuko walipo bila kufika ofisini
na vile vile watakuwa na uwezo wa kutumia mfumo kwa kutumia simu zao,”
alisema Dkt. Ndugulile.*
Amesema
Sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta muhimu katika Serikali ya Awamu ya
Tano ambapo sekta hiyo ni ya tatu kwa kupata bajeti kubwa.
Aidha ,kwa mwaka huu wa fedha jumla ya vituo vya afya 208 vimeboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya dharura ya mama na mtoto.
Dkt.
Ndugulile amesema ndani ya bajeti hii Hospital za wilaya 67 zitajengwa
nchini pamoja na hospitali za rufaa kwa mikoa ambayo haina hospitali ya
rufaa ya mkoa.
Wakati huo
huo, Waziri Ndugulile ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya (NHIF)
kufanya majukumu iliyopewa ikiwa ni pamoja kusajili vituo vyenye uwezo
wa kutoa huduma kutokana na vigezo vilivyowekwa na mfuko huo na
kuziachia mamlaka nyingine majukumu yake ya kukagua vituo hivyo kama
vile mikataba ya kazi ya wafanyakazi wa vituo husika.
Aidha,
ameutaka mfuko huo kutafakari juu ya masharti yaliyowekwa katika
kusajili vituo ambapo kituo hakiwezi kusajiliwa mpaka kiwe katika
uangalizi na mfuko huo kwa miaka isiyopungua mitatu.
Naye,
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Otilia Gowele amesema kanuni mpya
za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi zitasaidia kusogeza
huduma kwa wananchi pia hospitali hizo kutoa huduma kulingana na
mahitaji ya sasa
0 on: "WIZARA YA AFYA YAZINDUA MFUMO WA TEHAMA KWA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI."