Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika na mama yake katika Zahanati ya
Mwandiga ili kupata huduma za Afya wakati akikagua ubora wa huduma
zitolewazo katika Zahanati hiyo ikiwa ni siku moja kuelekea siku ya
Malaria Duniani katika Wilaya ya Kasulu Aprili 25.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akimsikiliza moja ya mama aliyekuja kipata huduma katika
Zahanati ya Mwandiga Mkoani Kigoma wakati akikagua ubora wa huduma
zitolewazo katika Zahanati hiyo kulia kwake ni Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Andy Karas.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akigawa vyandarua kwa mmoja wa mama wajawazito katika Zahanati
ya Mwandiga alipotembelea kukagua ubora wa huduma zitolewazo na Zahanati
hiyo, kulia kwake ni Mbunge wa Viti maalum Iringa Rose Tweve, anaefuata ni Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Andy Karas.
Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Andy Karas akitoa ujumbe kutoka makao makuu ya Shirika hilo kuhusu ugonjwa wa Malaria na namna ya kujikinga, ikiwa ni kuelekea siku ya Malaria Duniani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akisisitiza jambo kuhusu kinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria
katika Zahanati ya Mwandiga ikiwa ni kuelekea siku ya Malaria duniani
ambayo kitaifa itakuwa katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Kikundi cha burudani kutoka Mwandiga Wilaya ya Kigoma mjini mkoani Kigoma kikiburudisha wananchi waliojitokeza kumsikiliza mgeni rasmi katika Zahanati ya Mwandiga , mgeni rasmi ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kushoto kwake ni Mbunge wa Viti maalum Iringa Rose Tweve.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na wadau kutoka mashirika
mbali mbali wakiwa wamebeba mitungi ya kunyunyizia mazalio ya mbu
wanaosababisha ugonjwa wa Malaria.
Na WAMJW-KIGOMA
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeendelea na msisitizo wa vituo vya Afya, zahanati na hospitali za
Serikali kuacha tabia ya kuuza dawa za kutibu malaria nchini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea zahanati ya Mwandiga
iliyopo wilayani Kigoma katika kuangalia hali ya matibabu dhidi ya
Malaria wilayani humo kuelekea kilele cha siku ya Malaria Duniani.
"Nawaagiza
waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuweka matangazo
yanayoonyesha kipimo cha haraka cha Malaria , dawa Mseto za kutibu
Malaria kali ni bure kwenye kila vituo vya kutolea huduma za afya za
Serikali" alisistiza Waziri Ummy.
Aidha,Waziri
Ummy amesisitiza kuwa endapo mtoa huduma yeyote atakayemtoza mwananchi
malipo ya matibabu na vipimo vya Malaria hatua stahiki itachukuliwa
bila ya kumuonea huruma.
Waziri
Ummy amesema kuwa waganga wakuu wa vituo kwa ngazi ya zahanati na
waganga wakuu wa wilaya kuweka namba zao za simu kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya nchini ili kuwasaidia Watanzania kutoa malalamiko
yao pindi wanapopatiwa huduma ambazo za hazikidhi viwango ili kuendelea
kuboresha huduma za afya nchini.
Waziri
Ummy amesema kuwa katika kujikinga na Malaria wananchi wanatakiwa
kutumia vyandarua vyenye dawa, kusafisha mazingira na kuondoa mazalia ya
mbu waenezao ugonjwa huo kwani kinga ni bora kuliko tiba.
Sambamba
na hilo Waziri Ummy alitoa vyandarua vyenye dawa ya kukinga mbu
aenezaye Malaria katika kijiji cha Mwandiga ili kuendelea
juhudi za kutokomeza Malaria nchini katika kuelekea siku ya Malaria Duniani.
Aidha
Waziri Ummy ameshiriki zoezi la kunyunyizia viuatilifu pamoja na
kuzindua vikosi kazi vya kunyunyizia dawa hizo ili kuua viluilui
vinavyoweza kusababisha mazalia na ongezeko la ugonjwa wa malaria
katika kaya mbalimbali manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani humo.
Mbali
na hayo Waziri Ummy alijibu kero za wazee kuhusu vitambulisho vya
matibabu ambapo alisistiza mpaka Juni 15 mwaka huu vitambulisho hivyo
viwe vimepatikana kwa wazee wasiojiweza na katika Kijiji cha Mwandiga
Mkoani Kigoma.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa katika
kuhakikisha Malaria inatakiwa kujikita kwenye kinga ili kutokomeza
kabisa ugonjwa huo.
Siku
ya Malaria Duniani huadhimishwa kila Aprili 25 kila mwaka na
maadhimisho ya Mwaka huu yatafanyika wilayani Kasulu na kauli mbiu ya
mwaka huu inasema "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
0 on: "MARUFUKU KUUZA DAWA YA MALARIA. "