Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi uliofanyika mapema leo katika viwanja vya Mbagala Zakim jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimuakimkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi baada ya kukabidhiwa na wataalamu wa masuala ya Afya, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy (MB).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akikata utepe ishara ya uzinduzi rasmi wa Chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi shughuli iliofanyika mapema leo katika viwanja vya Mbagala Zakim jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipokea sindano ya chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi kutoka mtoa huduma za Afya, kulia ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy (MB).
Picha ya pamoja ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi
uliofanyika mapema leo katika viwanja vya Mbagala Zakim jijini Dar es
salaam.
Picha ya pamoja ikionesha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi waliohudhuria kumuunga mkono Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi.
NA WAMJW-DAR ES salaam
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amezindua chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi ili kutokomeza
vifo vitokanavyo na magonjwa hayo nchini.
Katika
ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan amesema kuwa chanjo hiyo imewalenga wasichana wote
wanaotimiza umri wa miaka 14 ili kuanza kujikinga mapema na ugonjwa
huo.
"Ili kupata kinga
kamili, wasichana watahitajika kupata dozi mbili ambapo dozi ya kwanza
itatolewa muda wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya
pili itatolewa miezi site baada ya kupata dozi ya kwanza" alisema Mhe.
Samiah Suluhu.
Aidha,Mhe.
Samia amesema kuwa chanjo hiyo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
inatolewa bila ya malipo pamoja na uchunguzi wake kwani Serikali
imedhamiria kutokomeza tatizo hilo nchini.
"Niwaagize
Waganga wa Mikoa na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa
mwaka ili kutoa huduma hiyo tena bila ya malipo kwa wanawake na
wasichana wote nchini" alisisitiza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu.
Mbali
na hayo Mhe. Samia Suluhu amesema kuwa takribani wasichana laki 616,
734 wanatarajia upata chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa
mwaka 2018 na chanjo hiyo imethibitishwa na Shirika la Afya
Duniani(WHO).
Kwa upande
wake Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu amesema kuwa chanjo hii itakuwa ya saba kati ya chanjo
ambazo zinatolewa kwa watoto ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali.
"Ukiacha
chanjo ya kukinga Saratani ya mlango wa Kizazi, hapa nchini chanjo
nyingine zinazotolewa ni ya kifua kikuu, Polio, Nimonia, Kuharisha ama
Rota, Surua na Rubella , Donda Koo, Kifaduro, Homa ya Ini, Uti wa mgongo
na Pepopunda kwa watu wazima" alisema Waziri Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imefanikiwa kuweka maghala
kuhifadhia chanjo katika mikoa yote nchini ambayo yana uwezo wa
kuhifadhi chanjo kwa miezi sita bila ya kuharibika.
Kwa
Mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa zawadi za fedha taslimu zitatolewa
kwa Mikoa mitatu itakayofanya vizuri katika utoaji wa chanjo ya kukinga
saratani ya mlango wa kizazi hapa nchini.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema
kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kutolea huduma za
afya ili kwenda kupata vipimo na chanjo za kukinga saratani pindi
wanapogundulika wana magonjwa hayo.
"Natoa
rai kwa wananchi mliojitokeza hapa kuwapeleka watoto zenu wake zenu na
wanawake wote hususan wasichana wenye umri wa miaka 14 kwenda kupata
chanjo hii na mkifika majumbani kwenu muwakumbushe watu wenu wa karibu
kushiriki katika upataji wa chanjo hii" alisema Mhe. Makonda.
0 on: "MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI"