Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee
na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wauguzi na wakunga hawapo
pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga
nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya
wawakilishi wa mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa
Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini
lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo akiongea na
wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la
Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wadau,wakunga na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la
Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wauguzi na Wakunga wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi
na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha uuguzi na Ukunga Dodoma wakiwakilisha
salamu zao kwa kutumia wimbo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani
wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini
lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Na WAMJW-Dodoma
Serikali imewataka Wauguzi na Wakunga nchini kufuata na kusimamia misingi ya maadili ya taaluma zao wakati wa kutoa huduma.
Hayo
yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa
Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini.
Najua
kuwa Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga inalishughulikia suala la
maadili kwa wauguzi na wakunga hivyo nitoe msisitizo tena huduma za
Uuguzi na Ukunga zinapimwa zaidi na uadilifu wa mtoa huduma hivyo
muendelee kusimamia kwa ukaribu misingi ya maadili ya taaluma zenu
amesema Dkt Ndugulile.
Aidha,
Dkt Ndugulile amewataka Wauguzi na Wakunga kupitia vyama vyao vya
kitaaluma kushirikiana na Baraza la Uuguzi na Ukunga kuendelea
kuwakumbusha mara kwa mara wauguzi kuhusu maadili ya taaluma yenu.
Mteja
anapokuja kwenye vituo vya kutolea huduma anategemea kupata huduma ya
upendo na huruma, anategemea kupewa maneno ya faraja na matumaini hivyo
basi, wale wote wanaoichafua taaluma yenu kwa kutotekeleza wajibu wao
kwa wakati, kuwadhalilisha, kuwashambulia au kutowasikiliza wateja wenu
wabainishwe na wahimizwe kujirekebishaamefafanua Dkt Ndugulile.
Ninawapongeza
sana kwa kuweka msisitizo kwa mambo yanayohusiana na kupunguza vifo vya
akina mama na watoto wachanga hiyo ni moja ya agenda muhimu ya Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dr John Pombe Magufuliameongeza Dkt. Ndugulile.
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa serikali inazifanyia kazi
changamoto zinazowakumba Wauguzi na Wakunga kwa namna mbalimbali ambapo
hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha bajeti kwa
ajili ya kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba, na
vitendanishi katika Bohari ya Dawa.
kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo
amesema kuwa kongamano hilo limeandaliwa ili kuwakumbusha wauguzi na
wakunga maadili ya taaluma yao pindi wanapokuwa sehemu zao za kazi.
Aidha
Bw. Moyo amesema kuwa Akizungumzia Kongamano hilo limebeba kauli mbiu
isemayo isemayo Kuelekea Huduma za Uuguzi na Ukunga Zinazozingatia
Ubora, Utu, Huruma na Usalama wa Wagonjwa; Katika Kupunguza Vifo vya
Akinamama na Watoto.
0 on: "WAUGUZI NA WAKUNGA WANATAKIWA KUZINGATIA MAADILI SEHEMU ZAO ZA KA"