Shekhe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Musa Salum akiishukuru Serikali
kupitia Wizara ya Afya kwa kujali Afya za wananchi, akiwa katika kikao
cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichoandaliwa
na Wizara ya Afya kupitia mpango wa chanjo.
Askofu Wa kanisa la mito ya baraka Bruno Mwakibolwa akichangia hoja
mbele ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe.Ummy Mwalimu na viongozi wengine wa dini (hawapo kwenye picha)
wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti
kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akitoa mapendekezo mbele ya viongozi wa dini waliokutana mapema
leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha kuhamasisha chanjo ya
mlango wa kizazi.
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akimkaribisha Mhe. Ummy Mwalimu ili
azungumze na viongozi wa dini.
Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo Dkt. Dafrossa Lymo akiwasilisha taarifa
kuhusu masuala ya chanjo nchini mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Viongozi wa Dini
(hawapo kwenye picha).
Viongozi wa dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu wakati wa kikao na
viongozi wa dini zote cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.
Viongozi wa dini ya kiislamu wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu wakati wa kikao na
viongozi wa dini zote cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akiwa na viongozi wa dini wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti
kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
Na WAMJW-Dar es
salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa kila mwaka
Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Saratani 50,000 huku Saratani ya
mlango wa kizazi ikiongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti na saratani ya ngozi.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu (MB) wakati wa mkutano na viongozi wa dini, uliofanyika mapema leo
katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam.
“Kila
mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wa Saratani wapya 50,000, katika
kila wagonjwa 100 wanaokwenda katika Hospitali ya Ocean Road wagonjwa 32
wanasaratani ya mlango wa kizazi, inafuatia saratani ya matiti ambayo takribani
wagonjwa 12 katika wagonjwa 100, saratani ya tatu ni saratani ya Ngozi” alisema
Mhe. Ummy Mwalimu.
Aliendelea
kusema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti zinachukua
takribani asilimia 45 ya wagonjwa wa saratani nchini, huku Saratani ya tezi
dume ikiwa na asilimia 2.
Kwa upande mwingine Mhe. Ummy
Mwalimu amewaomba viongozi wakuu wa madhehebu ya dini kuwahimiza wananchi
kuwapeleka wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kupata chanjo ya kuwakinga
na saratani ya mlango wa kizazi inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 Aprili,2018
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
jijini Dar es Salaam
Waziri Ummy amesema kwamba kama
viongozi wa dini ni vyema kufikisha ujumbe huu kwa waumini wao na kuwaunga
mkono ili kuweza kuwafikia wasichana laki 6 nchi nzima ili kuweza kuwaokoa na
vifo vipatavyo asilimia 50 vitokanavyo na saratani nchini"idadi hii ni
kubwa sana,hivyo juhudi na ushirikiano zaidi vinahitajika katika kupunguza vifo
hivi.
Hata hivyo aliwatoa hofu viongozi
hao pamoja na wananchi kwa ujumla kwamba chanjo hii haizuii binti kutopata
watoto katika maisha yake ya baadae bali ni kinga dhidi ya saratani ya mlango
wa kizazi". Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema tukashirikiana
kuweza kuwaokoa mabint wetu na vifo".
Chanjo mpya ya kuwakinga wasichana
wenye umri wa miaka 14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi itaanza
kutolewa mara baada ya uzinduzi wa kitaifa tarehe 10 Aprili, 2018 na itahusisha
mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar pia itatolewa kwenye vituo vyote vya
kutolea huduma za afya vya Serikali, binafsi na huduma mkoba kwenye shule na
sehemu mbalimbali. Chanjo hii itatolewa mara mbili ili kupata kinga
kamili(chanjo ya pili itatolewa baada ya miezi sita)
Kwa
upande mwingine Mhe. Ummy mwalimu alimshukuru Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt.
John Pombe Magufuli kwa kuongeza bajeti ya dawa za Saratani kutoka shilingi
Milioni 700 hadi Bilion 7 jambo lililosaidia sana katika matibabu ya Saratani.
“Nashukuru
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupandisha bajeti ya dawa za saratani
kutoka shilingi Milioni 700 hadi Billion 7, leo nasimama kifua mbele, angalau
katika wagonjwa 10, wagonjwa 7 watakwambia tumepata dawa bila malipo yoyote”
alisema Mhe. Ummy Mwalimu.
0 on: "TANZANIA YAPATA TAKRIBANI WAGONJWA WAPYA WA SARATANI 50,000 KILA MWAKA."