Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na mmoja ya wanawake
waliofika kupima Saratani ya mlango wa Kizazi katika kituo cha Ngamiani Mkoani
Tanga, wakati alipozindua Kampeni hiyo Mkoani hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya
wanawake na mabinti waliojitokeza katika kupima na kupata Chanjo ya Saratani ya
mlango wa kizazi iliyofanyika katika Kituo cha Afya Ngamiani Mkoani Tanga mapema
leo.
Kundi la Wanafunzi na Mabinti
waliojitokeza kumsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB), wakati alipozindua kampeni
ya Uchunguzi wa Saratani ya mlango wa
Kizazi na uhamasishaji kwa walezi na wazazi wa mabinti walio na umri wa miaka
14 kupata chanjo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijumuika na kikundi cha
Burudani cha ngoma cha Msanja kutoka Mkoani Tanga katika uzinduzi wa kampeni ya
Uchunguzi wa Saratani ya mlango wa
Kizazi na uhamasishaji kwa walezi na wazazi wa mabinti walio na umri wa miaka
14 kupata chanjo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimuunga mkono mmoja kati ya
wanafunzi waliofika katika kituo cha Afya Ngamiani kupata Chanjo ya Mlango wa
Kizazi mapema leo.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali na mabinti waliopata Chanjo ya Mlango
wa Kizazi leo katika Kituo cha Afya Ngamiani Mkoani Tanga.
Na WAMJW- TANGA
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imetoa msisitizo kwa watoa huduma za afya kutoa matibabu ya saratani ya
mlango wa kizazi bila ya malipo yeyote kwa wananchi.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya
mlango wa kizazi iliyofanyika leo Mkoani Tanga.
"Uchunguzi,
matibabu na chanjo ya kukinga Saratani ya mlango wa kizazi inatolewa
bila ya malipo yeyote katika vituo vya afya, zahanati na hospitali
zinazomilikiwa na Serikali" alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa ni lazima wazazi au walezi wa watoto wanaopata
chanjo waridhie ili kuweza kuwapa chanjo hiyo kwani kinga ni bora
kuliko tiba.
Kwa upande
wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Tanga Dkt. Malisely amesems kuwa lengo la
Mkoa wa Tanga ni kutoa Chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa
wasichana wapatao 38, 000 mkoani humo.
Aidha
Dkt. Malisely amesema kuwa ni lazima tuwaelimishe na tuwaeleze wazazi
umuhimu wa mtoto kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili
kujikinga na ugonjwa huo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini Bw. Thobias Mwilakwa amesema
kuwa wazazi na walezi wa Mkoa Tanga wanatakiwa kuwapeleka watoto wao
kupata huduma ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.
0 on: " MATIBABU YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NI BURE. "