Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipokea maelezo kutoka kwa
mwakilishi wa kianda cha kutengeneza vyandarua cha (A to Z) Textile Bw.
Slyvester Kazi wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo kwa
mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25 katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akiwa na viongozi wa Serikali na viongozi wa mashirika mbali mbali ya
kimataifa, wakiwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma
katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Mwakilishi kutoka mradi wa
upuliziaji wa dawa ya viuatilifu ukoko majumbani Bw. Christoper Mshana, akimpa maelekezo mgeni
rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo kwa mwaka huu
yanahadhimishwa leo Aprili 25 katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akionesha kitabu cha takwimu za Malaria pamoja na wadau mbali mbali wa sekta ya Afya kilichozinduliwa leo katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipokea ramani ya Tanzania inayoonesha mikoa iliyopungua ugonjwa wa malaria nchini kutoka kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Takwimu Tanzania (TBS) Dkt. Albina Chuwa.
Kikundi cha ngoma kutoka Umoja
Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kikiburudisha Viongozi na wananchi waliofika
katika viwanja vya Umoja ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo
kwa mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25 katika Wilaya ya Kasulu Mkoani
Kigoma.
Kundi la muziki wa Bongo fleva la
WEUSI wakiwa jukwaani kutoa Burudani na Elimu juu ya kinga ya ugonjwa wa
Malaria ambayo imehadhimishwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani
Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Kundi la wananchi lililojitokeza
katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya
siku ya Malaria duniani ili kusikiliza ujumbe kuhusu Malaria, mgeni rasmi wa
tukio hilo ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu (MB).
Na WAMJW- KASULU KIGOMA
KIWANGO
cha maabukizi ya ugongwa wa Malaria nchini kimeshuka kwa nusu zaidi
kutoka asilimia 14. 4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7. 3 mwaka
2017.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo
yamefanyika leo Wilayani Kasulu katika Mkoa wa Kigoma.
"Katika
kuhakikisha tunatokomeza kabisa ugonjwa huo Wizara ya Afya kupitia
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) tumepokea na kusambaza vitendanishi vya malaria
(mRDT) , vipimo 21, 428, 725, dawa za mseto dozi 12, 916, 050 kwa ajili
ya maralia isiyo kali, Sindano za kutibu Malaria kali vichupa 1, 668,
464 na vidonge vya SP dozi 6, 899, 700 kwa ajili ya tiba kinga dhidi ya
athari za malaria wakati wa ujauzito" alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa ili watanzania tuendelee kutokomeza kabisa
ugonjwa wa malaria watanzania wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika
kutumia afua zote za kupambana na ugonjwa huo ikiwemo kunyunyizia
viuadudu vya kuua viluilui vinavyoweza kuleta malaria.
Vilevile
Waziri Ummy amesisitiza kuwa kila Halmashauri za kila wilaya kuunda
kamati zitakazohamasisha usafi wa mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu
katika kutokomeza malaria.
Sambamba
na hilo Waziri Ummy amezindua takwimu za ugonjwa wa Malaria nchini
ambao umefanywa na Taasisi ya Takwimu nchini NBS ambayo ndio Takwimu
itayotumika na Serikali ya Tanzania.
Kwa
upande wake Waziri Wa Elimu na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema
kuwa atahakikisha wanafunzi wanapambana na ugonjwa wa Malaria kwa kuweka
somo la afya kwa shule zote za msingi na sekondari nchini.
Naye
Mkuu wa Mkoa Wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emamanuel Maganga
ametoa wito kwa wakazi wa kigoma kutumia vyandarua kwa matumizi sahihi
na siyo kinyume na hapo ikiwemo kufungia kuku na kuvulia samaki.
Kilele
cha Maadhmisho ya Malaria kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika
wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO
TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
0 on: "MALARIA YASHUKA MPAKA ASILIMIA 7. 3 NCHINI"