JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaomba viongozi wakuu wa madhehebu
ya dini kuwahimiza wananchi kuwapeleka wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14
kupata chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi inayotarajiwa
kuzinduliwa tarehe 10 Aprili,2018 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam
Waziri Ummy amesema kwamba kama
viongozi wa dini ni vyema kufikisha ujumbe huu kwa waumini wao na kuwaunga
mkono ili kuweza kuwafikia wasichana laki 6 nchi nzima ili kuweza kuwaokoa na
vifo vipatavyo asilimia 50 vitokanavyo na saratani nchini"idadi hii ni
kubwa sana,hivyo juhudi na ushirikiano zaidi vinahitajika katika kupunguza vifo
hivi.
Aidha, alisema hapa nchini kati ya
wagonjwa mia moja wa Saratani, wagonjwa 34 wana saratani ya kizazi".
saratani ya mlango wa kizazi inaongoza na inafuatiwa na saratani ya
matiti kwa asilimia 13 ya wagonjwa wa Saratani nchini"alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo aliwatoa hofu viongozi
hao pamoja na wananchi kwa ujumla kwamba chanjo hii haizuii binti kutopata
watoto katika maisha yake ya baadae bali ni kinga dhidi ya saratani ya mlango
wa kizazi". Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema tukashirikiana
kuweza kuwaokoa mabint wetu na vifo".
Chanjo mpya ya kuwakinga wasichana
wenye umri wa miaka 14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi itaanza
kutolewa mara baada ya uzinduzi wa kitaifa tarehe 10 Aprili, 2018 na itahusisha
mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar pia itatolewa kwenye vituo vyote vya
kutolea huduma za afya vya Serikali, binafsi na huduma mkoba kwenye shule na
sehemu mbalimbali. Chanjo hii itatolewa mara mbili ili kupata kinga
kamili(chanjo ya pili itatolewa baada ya miezi sita)
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-afya
6/4/2018
0 on: "TAARIFA KWA UMMA"