Wadau na Wafanyabiashara wa
Sekta ya Dawa wakifuatilia kwa umakini taarifa kutoka kwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha) katika kikao cha
kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya Dawa, tukio limefanyika mapema leo
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia hoja mbele ya Wadau
na Wafanyabiashara wa Sekta ya Dawa katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa
viwanda vya Dawa.
Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza jambo mbele ya wadau na
Wafanyabiashara katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda
uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika kikao cha Wadau wa
Sekta ya Dawa katika kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba
hapa nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Idara Kuu ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijageakiteta akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wake Prof. Elisante Ole Gabriel.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakiwa na Wadau
wa Sekta ya Dawa katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya Dawa
na vifaa Tiba hapa nchini.
Na WAMJW. Dar es salaam.
SERIKALI yawataka Wadau
wa Uwekezaji nchini kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika ujenzi wa
viwanda vya dawa ili kusaidia kupunguza gharama kubwa za matumizi zinazotokana
na kununua, kusafirisha na kuhifadhi dawa zinazotoka nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. UMMY
MWALIMU katika
kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa
nchini, kilichokutanisha
wadau mbalimbali wa Uwekezaji katika Sekta
ya Dawa, Vifaa na Vifaa tiba
Waziri Ummy alisema
kuwa Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya tirion moja kunuua dawa kutoka nje,
hivyo kupitia uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini itasaidia kupunguza adha
hiyo nchini kwa kiwango kikubwa.
Nae Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji nchini Mhe. Charles
Mwijage amewataka wote wenye nia
ya kuwekeza katika Ujenzi wa viwanda vya dawa, vifaa na vifaa tiba lazima
wahakikishe wanashirikiana na taasisi za Utafiti zilizopo nchini ili kuangalia
mahitaji na aina dawa zinazohitajika.
Aidha, Mhe.
Charles Mwijage amesema kuwa Uwekezaji na ujenzi wa Viwanda nchini utasaidia
kupunguza tatizo la ajira na kuchochea Maendeleo ya ukuaji wa Uchumi katika
ngazi ya watu na taifa kwa ujumla.
0 on: "SERIKALI YAWATAKA WAWEKEZAJI KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA UJENZI WA VIWANDA VYA DAWA"