Katika kipindi cha Mwaka 2017/2018, Wizara ilisimamia shughuli za utoaji wa chanjo kwa watoto ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa kitaifa na kimataifa yanafikiwa. Takwimu za Januari hadi Desemba 2017 zinaonyesha kuwa asilimia101.2 ya Watoto waliolengwa nchini walipatiwa chanjo zote muhimu ili kuwakinga na magonjwa. Mnamo mwezi Desemba 2017, Serikali yaTanzania ilipongezwa Shirika la Afya Duniani na wadau wa Kimataifa wa Chanjo kwa kufikia kiwango cha juu chachanjo kwa asilimia 97 ya uchanjaji watoto kwa chanjo ya pentavalent kwa takwimu za mwaka 2016. Lengo la Mkakati wa Dunia kupitia Shirika la Afya
Duniani ni nchi kufikia kiwango cha uchanjaji wa asilimia 90. Mikakati ya Wizara imewezesha nchi yetu kufikia kiwango hicho ambapo inakuwa nchi ya Tatu barani Afrika ikitanguliwa na Zambia yenye kiwango cha asilimia 99 ikifuatiwa na Rwanda yenye asilimia 98.

Hotuba nzima, bofya link ya chini hapa.
http://afyablog.moh.go.tz/2018/04/hotuba-ya-waziri-wa-afya-maendeleo-ya.html
0 on: "HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA AFYA 2018/2019"