Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akikagua kikosi cha timu ya Sabasaba wakati wa mchezo wa kumtafuta bingwa wa Mashindano ya kombe la Malaria wa Wilaya ya Kigoma mjini ambae atakutana na Bingwa wa Wilaya ya Kasulu ili kumpata Bingwa wa Mkoa wa Kigoma.
Wachezaji wa timu ya Sabasaba na timu ya Ujiji Fc wakigombea mpira katika viwanja vya Tanganyika Mkoani Kigoma wakati wa mashindano ya kombe la Malaria yaliyofanyika leo katika kuelekea siku ya Malaria duniani itakayofanyika Aprili 25 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleoya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akiongea na Wananchi
waliojitokeza kushuhudia mchezo kati ya Sabasaba na timu ya Ujiji Fc
katika kuelekea siku ya Malaria duniani itakayofanyika Aprili 25 mwaka
huu, yenye kauli mbiu ya "Nipo tayari kutokomeza Malaria, Wewe Je".
Afisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleoya
Jamii,Jinsia,Wazee na WatotoWinfred Mwafongo akimkabidhi zawadi ya jezi na mipira nohodha wa timu ya Saba saba walioibuka washindi katika mchezo huo wenye lengo la kuhamasisha watu kupambana na ugonjwa wa Malaria katika Mkoa wa Kigoma.
Na WAMJW-KIGOMA
MKURUGENZI
wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Leonard Subi amefungua mechi ya
fainali kati ya timu ya Sabasaba na Ujiji Fc kutoka Wilaya ya Kigoma
Mjini ili kumpata mshindi wa mashindano ya Malaria cup ngazi ya Mkoa katika kuelekea
maadhimisho ya siku ya Maralia Duniani.
Katika
ufunguzi huo Dkt. Subi amesema kuwa lengo la michuano hiyo ni
kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambapo mshindi wa
mchezo huo atachuana na mshindi atakayepatikana Wilayani
kasulu ili kumpata bingwa wa Mkoa wa Kigoma.
"Serikali
imedhamiria kuondoa ugonjwa wa malaria nchini hivyo wananchi wanatakiwa
kushirikiana kwa pamoja ili kutokomeza ugonjwa huo na tunatakiwa kwenda
kituo cha afya pindi unapohisi dalili za Malaria ili kupata vipimo na
kupata dawa kama utakua una maambukizi ya ugonjwa huo" alisema Dkt.
Subi.
Katika mchezo huo timu
ya Sabasaba iliibuka na ushindi kwa jumla ya magoli 2-1 dhidi ya Ujiji fc
hivyo kwenda kuchuana na timu ya Kasulu siku ya April 25 mwaka huu
katika Wilaya ya Kasulu.
Siku
ya Maralia duniani huadhimishwa April 25 kila mwaka na mwaka huu
maadhimisho hayo yatafanyika Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma huku Kauli mbiu
ya Maadhimisho hayo ni "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE? ".
0 on: "DKT. SUBI AFUNGUA MECHI YA FAINALI YA MASHINDANO YA KOMBE LA MALARIA, KIGOMA."