Na.WAMJW - DAR ES SALAAM
Serikali inatarajia kupata dola ya kimarekani
milioni 512 kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI kutoka Serikali ya Marekani
kupitia fungu la mradi wa dharura wa Rais
wa kupambana na UKIMWI Duniani.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa
akipokea rasmi taarifa ya kutolewa fedha za UKIMWI kwenye hafla iliyofanyika
kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa.
Dkt.Ndugulile alisema fedha hizo ambazo
serikali itapatiwa zitatumika kwa ajili ya kununulia dawa za kufubaza makali ya
Virus vya UKIMWI pia zitagawiwa kwa afua mbalimbali za kupambana na kuzuia maambukizi ya UKIMWI pamoja na
uhamasishaji wa upimaji wa Virus vya UKIMWI nchini.
Aidha ,alisema kiasi hicho cha fedha
zinatakiwa kutumika ndani ya mwaka mmoja kwa kwa kujikita kwenye malengo ya
Dunia ya tisini tatu(90,90,90) kwa
kuhakikisha kwamba asilimia 90 ya watanzania wote wanaohisiwa kuwa na Virusi
vya UKIMWi wanafikiwa,asilimia 90 ya wenye Virusi baada ya kupima wana pata
tiba na asilimia 90 wanaopata tiba kuweza kufumbaza Virusi vya UKIMWI.
Alisema kama nchi imekuwa na changamoto kubwa
sana na asilimia 90 ya kwanza ya upimaji
kutokana na Takwimu za mwaka jana za hali ya maambukizi nchini zinaonyesha bado
kuna changamoto kubwa hususan kwenye makundi ya vijana bado maambukizi
yanaongezeka hasa kwa wasichana”vilevile kwa upande wa wanaume ambao ni wagumu
kwenda kupima na wengine wanapima ila wanachelewa kuanza dawa na kutofuata
misingi ya umezaji dawa na hivyo kufa zaidi”.
“Mkakati ambao tunautafakari na kuja nao ni
ule wa mwananchi kuweza kujipima wenyewe kwa kutumia mate(Self-Test) hivyo kila
mtu aweze kujijpima mwenyewe kwa kwenda kununua kipimo duka la dawa kama ilivyo
kwa wanawake kujipima ujauzito”alisema Dkt.Ndugulile
Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwatoa hofu
wananchi kwamba Serikali haitawapima
wanaume kwa nguvu kwenye ma bar bali itatumika utaratibu ule ule katika makundi
yao kwa kuwapatia ushauri nasaha na kupima kwa hiari “hatusemi wanaume
watapimwa kwa nguvu hapana utaratibu utakua ule ule hivyo wananchi msipate hofu”
alisema dkt.Ndugulile
Alitaja mikakati mingine ni kwenda kuwafikia
makundi mahususi ambayo inaonekana yana maambukizi makubwa ikiwemo ya wavuvi pamoja na migodini hivyo
alitoa rai kwa watanzania kujitokeza ili kuweza kufikia asilimia 90 kutoka 52
ya upimaji wa Virus vya UKIMWI.
Naye Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt.
Inm alisema nchi yake ipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kujenga
Tanzania yenye afya nzuri.
0 on: " TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMWI"