Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akihoji ufanisi wa utendaji kazi wa moja ya mashine
ya kupima na kutambua dalili za mgonjwa mwenye EBOLA zilizopo Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Afya
Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George
Ndaki wakati alipofanya ziara katika Uwanja huo ili kujiridhisha na
utendaji na ufanisi wa mitambo ya kutambua dalili za mgonjwa mwenye
EBOLA.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiendelea na Ziara katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam akiongozana na mwenyeji
wake Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt.
Faustine akitoa maelekezo kwa Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki pindi alipofanya ziara leo
katika uwanja huo.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika eneo la
kupokelea mizigo wakati akiendelea na ziara yake, kulia kwake ni Afisa
Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George
Ndaki kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma za kinga Dkt. Khalid Massa
Picha ya muonekano wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam.
Na WAMJW-DSM
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
imeridhika na maandalizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko
ukiwemo ugonjwa wa Ebola katika mipaka yote na viwanja vya ndege nchini
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara
yake katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere
Dkt.Ndugulile
amesema amefika hapo ili kuangalia hali ya maandalizi na ufungaji wa
mashine za kisasa za utambuzi wa ugonjwa wa Ebola endapo itatokea mtu
mwenye ugonjwa huo
Aidha,
alisema wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa nchini na
kuweka mfumo wa kubaini watu wanaoingia kwa kubaini hali ya joto
linaloongezeka kwa mgeni anayeingia na kufanyiwa uchunguzi zaidi.
"tumeweka
mfumo wa kuwafuatilia wale ambao watakua wamebainika na joto zaidi
mahali watakapofikia na mawasiliano yao ili kujua hali zao na endapo
atapata mabadiliko"
Naibu
huyo aliongeza kuwa wamewafanyia mazoezi ya kutosha kwa watoa huduma wa
mipakani na viwanja vya ndege na pia kuwapatia elimu jinsi ya
kukabiliana na ugonjwa huo.
Dkt.Ndugulile
ameendekea kusisitiza na kuwatia hofu wananchi kwamba hadi sasa hakuna
mtu alobainika kuwa na ugonjwa wa Ebola na hali ya mipaka ya Tanzania ni
salama.
0 on: "SERIKALI IMEJIPANGA VIZURI KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO,IKIWEMO EBOLA, ASEMA DKT. NDUGULILE"