Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
chakula wanachopikiwa wazee wa kambi ya Nunge iliyopo Kigamboni wakati wa ziara
yake ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na
moja ya binti wa Mhitaji anaeishi katika kambi hiyo ya Nunge iliyopo Wilaya ya
Kigamboni, huku lengo la ziara hiyo likiwa kukagua hali ya utoaji huduma kituoni
hapo.
Baadhi ya Wazee waliojitokeza
katika ukumbi wa Kituo cha kulelea Wazee wa Nunge ili kupata fursa ya
kuzungumza na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pindi alipofanya ziara kituoni hapo.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza
na wananchi wake wa jimbo la Kigamboni Wilayani Kigamboni pindi alipofanya
ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
Na
WAMJW-DSM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeutaka uongozi wa Kambi ya Wazee
na watu wasiojiweza Nunge kuwakamata wahusika wanaouza viwanja katika eneo la
kambi hiyo .
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu
kero za Wazee wa Nunge alipotembelea kambi hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.
Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile
alisimamisha ujenzi wa nyumba ya mwananchi wan je na kambi hiyo uliokuwa unaendelea katika eneo hilo ambalo
inadaiwa sio muhusika wa eneo la kambi ya wazee ya Nunge na kusema aliyeuziwa
katika eneo hilo Serikali haitamtambua.
“Marufuku kwa mtu yeyote kuuza,kununua
wala kujenga pamoja na kuchimba mchanga
katika eneo la kambi hii na mtu atakayebainika anajihusisha na vitendo hivyo
basi hatua za sharia zitafuata zidi yake “ alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa
misaada inayokuja katika kambi hiyo iwe inawekwa kwenye utaratibu maalumu ili
kila mmoja aweze kupata mahitaji anayostahili kwa wakati husika na viorodheshwe
kwenye daftari la kambi hiyo kama kumbukumbu ili kuondoa changamoto ya
kurumbana kuhusu mahitaji kwa wazee hao.
Mbali na hayo Dkt. ametoa muda wa wiki mbili tatizo la usafiri
kwa wazee wa kambi hiyo liwe limeshughukulikiwa kwa kutengeneza bajaji
iliyotolewa na Serikali kwa manufaa ya Wazee wa kambi hiyo na si vinginevyo.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo
cha Afya cha kambi ya wazee Nunge Dkt.
Dismas Chihwalo wakati akisoma taarifa fupi ya kituo hiko amesema kuwa ili
uwepo utaratibu mzuri wa kuhudumia walengwa katika kambi hiyo ni lazima kuwepo
na makualiano maalumu kwa kutia saini baina ya wanaoletwa kwa mahitaji maalum
na viongozi wa kambi hiyo.
“Serikali inatakiwa kuhakikisha
wanaoletwa kwa ajili ya huduma maalum na kwa muda maalum wanatia saini mkataba
wa makubaliano ili kuweza kuepusha migogoro ya kutoa huduma katika kambi hiyo
kwa wanaostahili” alisema Dkt. Chihwalo.
Kambi ya Wazee na wasiojiweza Nunge
ilianzishwa mwaka 1936 kwa makusudi ya kuwahudumia Wazee na wasiojiweza pamoja
na wenye ukoma ili wasipate shida za mahittaji muhimu na huduma za afya kwa
wakati sahihi.
0 on: "WANAOHUSIKA NA KUUZA VIWANJA KATIKA ENEO LA KAMBI YA WAZEE NUNGE WAKAMATWE."