Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza moja kati ya Wataalamu wa Picha za Mionzi kwenye jengo la Mionzi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar Es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwajulia hali Wagonjwa waliofika kupata Huduma za Afya katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Jijini Dar es salaa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Mgonjwa aliyetoka nchi ya Jirani ya Kenya kupata matibabu Kansa nchini katika Taasisi ya Ocean Road Jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua vifaa ambavyo vimenunuliwa na Serikali kwa
gharama ya shilingi Bilion 9.5, alipofanya Ziara katika Taasisi ya Ocean Road jijini Dar es salaam. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage.
Baadhi ya Mitambo ya Mionzi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyogharimu jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 9.5.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza msafara wa kukagua hali ya utoaji huduma za Afya, na kukagua vifaa ambavyo vimenunuliwa na Serikali kwa
gharama ya shilingi Bilion 9.5. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Julius Mwaiselage.
OCEAN ROAD YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 7.5 KWA MWAKA.
Na WAMJW-DSM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imefanikiwa kuokoa zaidi ya Bilion 7.5 zilizokuwa zikitumika kwaajili ya
matibabu ya Wagonjwa wa Saratani nje ya nchi.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipofanya ziara ya kukagua hali ya
utoaji huduma katika Taasisi ya Ocean Road na kukagua vifaa ambavyo vimenunuliwa na Serikali kwa
gharama ya shilingi Bilion 9.5.
Dkt.
Ndugulile aliendelea kusema kuwa vifaa hivi (Linac Mashine na CT
Similator) vinaifanya nchi ya Tanzania kuwa moja kati ya Nchi chache
barani Afrika ambayo inavifaa vya kisasa katika kutibu wagonjwa wa
Saratani.
“Mashine hizi
ambazo zipo ndani ya majengo haya yamenunuliwa na Serikali ya awamu ya
Tano kwa gharama ya Shilingi Bilion 9.5, Vifaa hivi vinaitwa Linac
Mashine na CT Similator vinaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi
chache sana Barani Afrika ambazo zinavifaa vya kisasa zaidi kwaajili ya
matibabu ya Saratani” Alisema Dkt. Ndugulile
Pia,
Dkt. Ndugulile alisema kuwa Vifaa hivi vyenye ufanisi mkubwa vinasaidia
sana katika kuongeza idadi ya Wagonjwa kupata matibabu kutoka wagonjwa
170, mpaka 270 kwa siku, huku ikipunguza muda wa wagonjwa kusubiria
matibabu kutoka wiki 6 mpaka chini ya wiki 2.
Aidha,
Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inajipanga kufunga kifaa kikubwa
cha Pate Scan ambacho kitasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa wa Saratani.
Akisoma
Risala ya Taasisi hiyo Mkurugenzi wa Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage
alisema kuwa gharama za ujenzi wa jengo la vifaa vifaa hivo ni shilingi
Bilion 2.3 ambazo zote zilitolewa na Serikali.
“Gharama
ya ujenzi huu ni shilingi Bilion 2.33 ambapo zilitolewa zote na
Serikali, Jengo hili limekwishakamilika, na liliweza kufanyiwa uhakiki
na Tume ya Nguvu za Atomic Tanzania, pamoja na shilika la kimataifa la
nguvu za Atomic walilipitia na kuliangalia vigezo vyake kama vimefikiwa
na waliona vinafaa”. Alisema Dkt. Mwaiselage.
Mbali
na hayo Dkt. Mwaiselage alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kugharamia Mradi huo uliogharimu
jumla ya shilingi Bilion 9.5, zilizojumuhisha gharama za kupeleka
Wataalamu kwaajili ya kupata mafunzo nje na ndani ya nchi.
“Mradi
ulikuwa na sehemu ya Mafunzo kwa Wataalamu nje na ndani ya nchi, jumla
ya gharama ya mradi huu ilikuwa ni Bilion 9.5, na fedha zote hizi,
ziligharamiwa na Serikali chini ya Raisi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
na tunamshukuru sana kwa kuweza kutoa fedha kwaajili ya mradi huu”.
Alisema Dkt. Mwaiselage.
0 on: "OCEAN ROAD YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 7.5 KWA MWAKA"