Kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua
kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Najma Giga
aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua
kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa taarifa juu ya jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Bunge jijini Dododma.
Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba akitoa Elimu Mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na Jitihada mbali mbali za kudhibiti ugonjwa huo katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua
kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
Bi. Agatha Chikoti aliewai kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu na kupona kabisa akitoa ushuhuda mbele ya Wabunge katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua
kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Mgeni rasmi ambae ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh.
Najma Giga
aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kikao cha Uzinduzi
wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa
kifua
kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
WABUNGE WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU NCHINI.
Na WAMJW-DODOMA
Wabunge
nchini wamehamasishwa kushiriki katika kuongoza juhudi za kutokomeza
ugonjwa wa kifua kikuu (TB) ambao unaonekana kuwa tishio kubwa.
Hayo
yameelezwa na mbunge wa viti maalumu (CCM) Mh. Najma Giga
aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika uzinduzi wa
mtandao wa wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua
kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
Mhe.
Giga amesema kuwa ni wajibuwa kila mbunge nchini kuisimamia serikali
ili ishughulikie kikamilifu tatizo la kifua kikuu kwa kutenga rasilimali
za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari.
“Kifua
kikuu kinaleta madhara kiafya na huongeza umasikini katika jamii,
takribani watu 154,000 uugua kila mwaka na 27,000 ufariki duniani ikiwa
ni sawa vifo 74 kwa siku, hii inaonesha ni jinsi gani ugonjwa wa TB ni
hatari na hivyo juhudi za ziada zinahitajika ili kuutokomeza”. Amesema
Mh. Giga.
Aidha Mh. Giga
ameipongeza serikali na wataalamu wa afya kwa kuweza kuchunguza na kutoa
matibabu kwa wagonjwa wa kifua kikuu na kuhakikisha wagonjwa wanapata
matibabu bure na wanapona kabisa katika hospitali zote nchini.
Mh.
Najma amesema kuwepo kwa mtandao wa wabunge wa kupambana na TB nchini
(Parliamentary TB Focus) kutawezesha kufikia malengo ya kimataifa na
kitaifa ya kutokomeza TB kwa kutambua kuwa ni janga la kitaifa.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema wizara hiyo inatoa kipaumbele juu
ya ugonjwa wa TB kwa kufanya juhudi kubwa ya kuutokomeza ugonjwa huu
nchini ikiwemo kuweka teknolojia za kisasa za mashine za Genex part
zaidi ya 209.
“Jambo
ambalo tumelifanya kama serikali ni kujaribu kufanya utaratibu tofauti
wa jinsi gani ya kufanya upimaji wa ugonjwa huu. Hadi hivi sasa tumeweka
teknolojia za kisasa za mashine za Genex part zaidi ya 209 nchi nzima
ambazo utoa majibu ndani ya masaa mawili”. Alisema Dkt. Ndugulile.
Pia
Dkt. Ndugulile amesema kuwa dawa zote zinazotibu kifua kikuu cha
kawaida na kifua kikuu sugu zinapatikana nchini na matibabu yake pamoja
na vipimo vyote vinavyohusiana na ugonjwa wa TB yanatolewa bure.
Sambamba
na hayo, Shuhuda Bi. Agatha Chikoti aliyewahi kuugua ugonjwa wa kifua
kikuu ameiasa jamii kuacha kwenda kutafuta dawa za kienyeji na badala
yake kwenda hospitali kupima na kupewa tiba sahihi.
0 on: "WABUNGE WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU NCHINI."