Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhamad Bakari Kambi (Wakwanza Kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu wakiwa katika matembezi ya Hiari ya kuelimisha
na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yalipoanzia
katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Karimjee jijini
Dar es salaam.
Kikundi Shupavu cha Vijana wa Skauti kikiwa kimeshika Bango lenye maandishi ya kutoa Elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola wakati wa matembezi ya Hiari ya kuelimisha
na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yalipoanzia
katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Karimjee jijini
Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwongozo utaosaidia jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika nchi yetu endapo utainia nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akiwa ameshika Mwongozo utaosaidia jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika nchi yetu endapo utaingia nchini.
WAKUU WA MIKOA NCHINI WATAKIWA KUTENGA VITUO MAALUM VYA KUHUDUMIA WAGONJWA WA EBOLA.
Na WAMJW - DSM
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu amewataka Wakuu wa mikoa wote kutenga vituo maalumu katika kila
halmashauri cha kuhudumia na kuhifadhi wagonjwa wa Ebola endapo
wataingia nchini.
Waziri
Ummy Ameyasema hayo mapema leo katika Matembezi ya Hiari ya kuelimisha
na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yalipoanzia
katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Karimjee jijini
Dar es salaam.
"Lazima
kila mikoa, Halmashauri kutenga kituo maalumu cha kuhudumia wagonjwa wa
Ebola endapo watatokea, katika kila mkoa, kila Wilaya lazima wawe na
chumba maalumu kwaajili ya kuhifadhi wagonjwa wa Ebola endapo wataingia
"alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha,
Waziri Ummy aliwaomba Viongozi wa Dini kutumia majukwaa yao katika
Maubiri yao kutoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ugonjwa huu wa Ebola,
huku akiwaomba wasanii na viongozi wa Siasa nchini kutumia majukwaa yao
ili kutoa madaraja kufikisha taarifa kwa wananchi.
Kwa
mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa licha ya ugonjwa wa Ebola
kutoingia nchini, bado tupo katika hatari kubwa ya kuupata ugonjwa huu
kutokana na muingiliano wa wananchi baina ya nchi ya Tanzania na eneo la
Kivu Kaskazini ambalo ni karibu na nchi ya Tanzania.
"Ebola
bado haijaingia nchini Tanzania, lakini ni Kweli Kwamba tupo katika
hatari kubwa zaidi kupata Ugonjwa huu wa Ebola, hii inatokana Na mlipuko
wa ugonjwa huu kuwepo katika eneo la Kivu Kaskazini ambalo ni karibu na
nchi ya Tanzania na kutokana na muingiliano wa wavuvi baina ya nchi
hizi", Alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy alisema kuwa Tanzania inaweza kuzuia ugonjwa wa Ebola
usiingie nchini kwa vitengo vinavyihusika kutoa elimu na uelewa
wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola, itakuwa ni moja ya njia kubwa ya
kuzuia ugonjwa huu usiingie.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO watu 111
wametolewa taarifa kuugua ugonjwa huu wa Ebola na watu 75 sawa na
Asilimia 67% wamefariki kutokana na ugonjwa huu, vifo ni zaidi ya
Asilimia 50%. Maana yake kukiwa na wagonjwa 100, tunapoteza wagonjwa 50.
"Kwa
mujibu wa Takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO) Mpaka sasa, watu 111
wametolewa taarifa ya kuugua ugonjwa huu wa Ebola, watu 75 sawa na
Asilimia 67% wamefariki, ndiomaana tunaogopa sana kama tutaruhusu
ugonjwa huu utaingia nchini, vifo ni zaidi ya Asilimia 50%, maana yake
tukiwa na wagonjwa 100 , tunaweza kupoteza wagonjwa 50, kwakweli
tusikubali ugonjwa huu kuingia nchini "Alisema Waziri Ummy .
.
0 on: "WAKUU WA MIKOA NCHINI WATAKIWA KUTENGA VITUO MAALUM VYA KUHUDUMIA WAGONJWA WA EBOLA."