Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongea na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya,
kutoka Sekta Binafsi na Sekta za Serikali wakati wa ufunguzi wa mkutano
wa pili wa mwaka wa Sekta Binafsi na Sekta za Serikali.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha Mgeni
rasmi katika Mkutano wa pili wa mwaka wa masuala ya Afya jlioshirikisha
Sekta Binafsi na Sekta za Serikali leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Kutoka Sekta Binafsi Bw. akiongea na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya,
kutoka Sekta Binafsi na Sekta za Serikali wakati wa ufunguzi wa mkutano
wa pili wa mwaka wa Sekta Binafsi na Sekta za Serikali.
Wadau mbali mbali kutoka Sekta Binafsi na Sekta za Serikali walioshiriki
katika Mkutano wa pili wa mwaka wa Masuala ya Afya uliofanyika katika
ukumbi wa Bank Kuu ya Tanzania (BoT) leo jijini Dar es salaam
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kufungua Mkutano wa pili wa mwaka wa masuala ya Afya jlioshirikisha
Sekta Binafsi na Sekta za Serikali leo jijini Dar es salaam.
DKT. NDUGULILE AHIMIZA USHIRIKIANO WENYE MATOKEO YANAYOONEKANA BAINA SEKTA BINAFSI NA SEKTA ZA SERIKALI.
Na WAMJW- Dar es salaam
NAIBU
WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amehimiza ushirikiano wa karibu wenye tija na matokeo
yanayoonekana baina ya Sekta Binafsi na Sekta za Serikali katika kuleta
Maendeleo chanya kwa wananchi.
Amesema
hayo mapema leo wakati akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa Sekta
binafsi na Sekta ya Serikali uliofanyika katika ukumbi wa Bank kuu ya
Tanzania (BoT) jijini Dar ea salaam.
Dkt.
Ndugulile alisema kuwa katika kuboresha Sekta ya Afya nchini, Serikali
inahitaji ushirikiano wa karibu na Sekta Binafsi ili kurahisisha utoaji
wa Huduma za Afya kwa wananchi, huku akisisitiza matokeo yanayoonekana
katika ushirikiano wa pande hizo .
"Kusudio
la Serikali ni jema kabisa, na ndomana tumeweka Sera na Sheria, sisi
kama Serikali hatuwezi kuyafanya yote, tunahitaji Sekta ya Binafsi
tushirikiane, Serikali iliyopo saivi madarakani inataka matokeo, hatupo
hapa kukutana kila mwaka wakati hatuna mradi ulioshirikisha pande zote"
alisema Dkt. ndugulile.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile ameagiza watumishi wote wa Sekta ya Afya
nchini kuacha ubabaishaji pindi Sekta Binafsi zinapohitaji ushirikiano
katika kuleta Maendeleo kwa wananchi na kuagiza kumchukulia hatua yeyote
atakaebainika kutenda kosa hilo.
"Niwaombe
sana wafanyakazi wenzangu wa Sekta ya Serikali tuache urasimu,
tuangalie jinsi gani yakurahisisha ushirikiano ili mawazo mazuri yalete
Maendeleo, tunataka kuwekeza katika viwanda, bado tunahitaji Huduma
zakibingwa, watu wapo tayari, nataka tuache vikwazo", alisema Dkt
Ndugulile
Pia, Dkt
Ndugulile alitoa ushauri kwa Afisa Tabibu juu ya namna yakudhibiti
matumizi ya fedha nyingi ambayo yanatumika kununua vifaa vya matibabu na
mashine za maabara na thieta kwa kutoa fursa kwa Sekta Binafsi kununua
na kuendesha mashine hizo huku Serikali ikijikita katika kutoa Huduma
zilizo bora kwa wananchi.
"Sioni
sababu ya Serikali kuingia gharama za kununua vifaa vya kutibu, maabara
na thieta, kwanini tusiweke utaratibu wa watu wa Sekta Binafsi,
wawekeze kwenye vifaa, sisi kama Serikali tujikite katika kutoa Huduma,
itatusaidia sana sisi kutoa Huduma bora" alisema Dkt Ndugulile.
Dkt.
Ndugulile aliendelea kusisitiza kwamba , Sekta Binafsi si washindani
wala maadui wa Sekta za Serikali hivyo ni lazima kuhakikisha ushirikiano
unakuwa katika kutoa Huduma bora kwa wananchi, hivyo kutoa mwanya kwa
yoyote mwenye wazo zuri ikiwemo ujenzi wa viwanda vya dawa kuleta wazo
hilo ofisini kwake na kuahidi kulitekeleza Mara moja.
Sambamba
na hilo Dkt Ndugulile alisema kuwa Serikali imedhamiria kuja na Sera
ambayo itamtaka kila Mtanzania kuwa na Bima ya Afya ili aweze kupata
Huduma za Afya, hivyo kuwataka Sekta Binafsi kuja na mawazo jinsi gani
inaweza kushiriki katika kufanikisha wazo hili.
0 on: "DKT. NDUGULILE AHIMIZA USHIRIKIANO WENYE MATOKEO YANAYOONEKANA BAINA SEKTA BINAFSI NA SEKTA ZA SERIKALI"