Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali kutoka Wizara ya Afya
wakifuatilia kwa makini mawasilisho kutoka kwa wawezeshaji wa mkutano wa
Waganga wafawidhi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jijini
Dodoma.
Baadhi ya Waganga Wafawidhi kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia kwa
makini mawasilisho kutoka kwa wawezeshaji wa mkutano wa Waganga
wafawidhi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wawasilishaji wa mada mbalimbali wakiwasilisha mada kwa
waganga wafawidhi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Waganga afawidhi
uliofanyika jijini Dodoma.
WAGANGA WAFAWIDHI NCHINI WATAKIWA KUWEKA VIKAO KUJADILI VIFO VYA UZAZI
Na WAMJW- DODOMA
WAGANGA
Wafawidhi nchini wametakiwa kukaa vikao kila baada mara kwa mara ili
kujadili sababu ya vifo vinavyotokea kwenye hospitali zao ili kuzifanyia
kazi changamoto hizo na kurudisha taarifa Wizara ya Afya.
Hayo
yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Wizara ya
Afya Dkt. Otilia Gowelle wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waganga
Wafawidhi nchini uliofanyika leo jijini Dodoma
“Waganga
Wafaidhi mnatakiwa kukaa vikao vya kitabibu kujadili tiba pamoja na
kujadili kifo cha kila mgonjwa ili kujua changamoto iliyotokea na
kuipatia ufumbuzi na kuandikia taarifa ili kuondokana na vifo hasa
vitokanavyo na Uzazi” alisema Dkt. Gowelle.
Aidha,
Dkt. Gowelle amewataka wataalam wa tiba kuzingatia vikao vya tiba na
kufanyia kazi changamoto au maboresho ili kuzitolea taarifa na kuzitatua
pamoja na kushirikisha wadau wengine.
Dkt. Gowelle
amewataka pia Waganga wafawidhi kuweka mifumo ya ufuatiliaji wagonjwa
pamoja na kupokea malalamiko katika hospitali zao ili kufanya maboresho
ya huduma za afya wanazozitoa na kuchukua hatua zinazostahili.
“Kupitia
kikao hiki, nawataka mkae kama timu na kuandaa Mipango kazi ya kuanza
kushughulikia kikamilifu yale yote yaliyobainika katika taarifa hiyo ili
kuondokana na kero wanazokabiliana nazo wananchi wanapokuja kupata
huduma katika hospitali zenu” alisema Dkt. Gowelle.
Aidha,
Dkt. Gowelle amewasihi Waganga Wafawidhi waliohudhulia kikao hiko
kuhakikisha kwamba wanatumia timu zao za Uendeshaji za Hospitali za
Rufaa za Mikoa kubaini changamoto zilizopo katika maeneo yenu ya kazi
ikiwa ni pamoja na watumishi, majengo na vifaa vya kuzifanyia kazi ili
kuboresha huduma mnazotoa kwa wananchi.
Mbali na
hayo Dkt. Gowelle ametoa pongezi kwa timu yote ya inayoratibu
utekelezaji wa Mradi wa RRHMP pamoja na Serikali ya Japan kupitia
Shirika la Maendeleo JICA kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania
katika kuboresha huduma za Afya nchini.
0 on: "WAGANGA WAFAWIDHI NCHINI WATAKIWA KUWEKA VIKAO KUJADILI VIFO VYA UZAZI"