Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 13 Oktoba 2018

DKT NDUGULILE AGAWA KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WASANII ZAIDI YA 100


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndungulile akisema jambo katika mkutano wa Umoja wa Wasanii wa Muziki uliofanyika katika ukumbi wa NSSF Ilala, Jijini Dar es salaam.
  
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (katiki mstari wa chini) katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano Umoja wa Wasanii wa Muziki uliofanyika katika ukumbi wa NSSF Ilala, Jijini Dar es salaam huku akiwa ameshika sampuli za kadi ya bima ya afya.

Wadau wa mkutano wa Umoja wa Wasanii wa Muziki wakisikiliza mada.


Na. WAMJW - DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Dkt Faustine Ndugulile, leo tarehe 13/10/2018 ameshiriki katika mkutano wa Umoja wa Wasanii wa Muziki uliofanyika katika ukumbi wa NSSF Ilala, Jijini Dar es salaam.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Kadi hizo za bima ya Afya Mhe Ndugulile mewataka wasanii kutumia vipaji vyao kuelimisha jamii hususani katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii kama unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

Vilevile amewahasa wasanii kuzingatia maadili ya taifa katika kufanya kazi zao kwani wapo waimbaji ambao wamekuwa wakikiuka maadili na nyimbo zao zinapofungiwa wanalalamika bila kujua kuwa wao ndio wenye makosa.

Akijibu ombi la wasanii kuwapa kipaumbele cha bei nafuu ya bima ya afya, Mhe. Ndugulile amesema kuwa kwa kuzingatia kuwa kugharamia huduma za afya ni changamoto, serikali imetoa maelekezo kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuweka vifurushi rafiki kwa wananchi wa kawaida vitakavyoendana na mahitaji ya mwananchi mmoja mmoja kuchagua kulingana na Mahitaji yake.

Aidha, Mhe Ndugulile amesema serikali ikitoa sera mpya ya afya itamtaka kila mwananchi kujiunga na bima ya afya kwa lazima ili watu wote waweze kupata matibabu kwa urahisi pindi wanapoenda katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Akizungumzia matibabu bure kwa wazee, Mhe Ndugulile amesisitiza kuwa katika Sera Mpya ya Afya itakayotolewa na serikali itaboresha zaidi na kuweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wazee kwani kutokana na utafititi uliofanywa na Wizara, magonjwa mengi ya wazee ni yale ambayo yanajulikana na mara nyingi si ya kuambukiza.

Pia amewataka Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuendelea kubaini changamoto na kufanya maboresho ya namna bora zaidi ya kuwapatia bima za afya wananchi hasa wale ambao hawako katika mfumo rasmi wa ajira.

0 on: "DKT NDUGULILE AGAWA KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WASANII ZAIDI YA 100"