“Utumiaji wa mihadarati kuwa ni
changamoto kubwa inayowakabili vijana katika mataifa yote pia utumiaji wa
madawa ya kulevya na pombe vimehusishwa kwa kiasi kikubwa na tabia hatarishi ya
ngono zembe na ajali za barabarani” alisema Prof. Kambi.
Prof Kambi amesema kuwa sambamba na elimu kwa Umma Wizara itaendelea kutoa matibabu ya afya ya
akili katika hospitali zote za Umma nchini pamoja na kuendelea kutoa dawa za
Methadone kwa watumiaji wa madawa ya kulevya katika mikoa ya Dar es
salaam,Mbeya,Mwanza na Dodoma hivi
karibuni.
Aidha Prof. Kambi amesema kutokana na
tafiti za shirika la afya duniani (WHO) zinaonesha vijana wanaoathirika na
kupata matatizo ya akili ni wale walio katika umri wa kuanzia miaka 14, lakini wengi
wao hawapati nafasi ya kutambulika na kupata matibabu katika wakati muafaka.
“Tafiti za shirika la afya duniani
(WHO) zinaonesha takribani nusu ya magonjwa yote ya akili huanzia katika umri
wa miaka 14 ambapo magonjwa ya akili na matumizi ya vilevi ni miongoni mwa
changamoto kubwa sana za kiafya na kiusalama zinazoathiri rika hili la
binadamu”. Amesema Prof. Kambi.
Prof. Kambi amesema kuwa kujiua kunaaminika kuwa ni chanzo kikuu cha
pili cha vifo vyote vinavyowakabili vijana wengi duniani ambapo Ugonjwa wa
Sonona (Depression) umetajwa kushika nafasi ya tatu duniani katika magonjwa
yote yanayoathiri vijana duniani.
Kwa mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa
Takwimu za mwaka 2015 hapa nchini zinaonesha vijana kuanzia miaka 13 hadi 17 walioko katika shule za misingi na
sekondari zinaonesha kuwepo na dalili za Sonona, ambapo vijana zaidi ya
asilimia 7 walionyesha kuwa na dalili hizo
Kwa upande wake mtaalamu wa magonjwa
ya akili kutoka Hospitali ya Milembe Dkt. Damas Andrew kuwa matatizo ya unywaji pombe na uvutaji wa sigara
yalitaarifiwa kwa kiwango sawa cha asilimia 5, huku asilimia 3.1 wakiripotiwa kuvuta bangi katika maisha yao huku utafiti
huo ulionesha kuwa robo ya vijana wote waliohojiwa waliripoti kufanyiwa uonevu
na wenzao.
“Vijana wote waliohojiwa waliripoti
kufanyiwa uonevu na wenzao ama kwa kupigwa, kusukumwa au kufungiwa madarasani
kunakopelekea kupata athari ya akili”. Amesema Dkt. Damas
Dkt. Damas amesema utafiti umeripoti
kuwepo kwa matukio mbalimbali ya ukatili kwa vijana kutoka kwa wazazi na walezi
yanayosababisha kuzorotesha ya akili kwa watoto na vijana wanaowalea. Vilevile
kiwango kikubwa cha unyanyasaji kimeripotiwa kufanyika katika mitandao ya
kijamii dhidi ya watoto na vijana na kufanya changamoto hizi kuathiri kwa kiasi
kikubwa afya ya akili.
0 on: "VIJANA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA ILI KUEPUKA ATHARI ZA AFYA YA AKILI"